WATENDAJI WA SERIKALI WAAGIZWA KUWALINDA WAWEKEZAJI WAZAWA
byJohn Banda-
0
Serikali imewataka viongozi wa
kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia madaraka yao vibaya
kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi.
Aidha viongozi hao wametakiwa
kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki yatakayowawezesha kufanya
biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza
ajira kwa vijana.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda
mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa
mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa.
Prof. Mkenda amewasihi viongozi
wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya nchini kujivunia uwepo wa
wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazawa kwani wao ni
chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara (anayetazama kamera) akibadilishana mawazo na baadhi ya
viongozi wa mkoa wa Simiyu nje ya ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi
wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji na tovuti ya mkoa wa Simiyu.(Picha zote na Thebeauty.co.tz).
Amesema kuwa si vyema
wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha zisizokuwa sahihi na kuonekana
kama wana uadui na serikali, na badala yake watukuzwe ili kuweza kulipa
kodi pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi.
“hawa wafanyabishara hasa wazawa
na wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu zetu na watu muhimu, kwani
wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi ipate maendeleo, lakini
wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
tuwathamni” alisema Prof.Mkenda.
Katibu Mkuu huyo amezitaka
halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya
wawekezaji wakubwa na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akisaliana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Festo S. Kiswaga mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Kanisa
Katoliki Bariadi, mkoani Simiyu kushiriki uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji mkoani humo pamoja na kuzindua tovuti ya mkoa huo.
Awali akizungumza katika sherehe
hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amesema kuwa ili Tanzania iweze
kufanikiwa katika azma yake ya kuwa na viwanda lazima serikali iwekeze
kwanza katika utafiti wa fursa zilizopo.
Amesema kuwekeza katika utafiti
utasaidia kutoa uthubutu wa kufanya na kutenda mambo mbalimbali
yatakayoifanya nchi kuwa na uchumi wa kati na kuwaletea wananchi
maendeleo.
“nchi hii tusingelihitaji kuona
wakuu wa mikoa kuwa wabobezi katika kila sekta na badala yake wawaache
wataalam na watafiti wafanye kazi zao kitaalamu ili kuepuka mvurugano wa
shughuli za kimaendeleo ndani ya nchi” amesema Mtaka
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akitoa utambulisho wa meza kuu
na maelezo ya lengo la mwongozo wa uwekezaji katika sherehe hizo
zilizofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.
Kwa upande wake Taasisi ya Utafiti
wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda, amesema kukamilika
kwa utafiti huo mkoani Simiyu utatoa fursa kwa wananchi na
wafanyabishara kutambua wapi kuna fursa sahihi na haraka kuwekeza.
Utafiti huo ulifanywa na Taasisi
ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) kati ya mwezi Januari na Februari
mwaka huu mkoani humo kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) ambapo zaidi ya shilingi Milioni 60 zilitumika katika
utafiti huo na kubaini uwepo wa fursa 26.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni
rasmi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani
humo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mwongozo
wa uwekezaji mkoani Simiyu ulioenda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya
mkoa wa Simiyu.Mtafiti
wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda
akitoa wasilisho la fursa za uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe
za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.Mtafiti
wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda
akiitambulisha timu iliyoshiriki kwenye utafiti huo. Kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF),
Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi.
Margareth Nzuki, Afisa wa Habari Mwandamizi wa ESRF, Abdallah Hassan
pamoja na UNDP Programme Specialist, Amon Manyama.Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini ambao
ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo akitoa salamu za UNDP wakati wa
sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu.Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa salamu za ESRF wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa
uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki
Bariadi.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Antony Mtaka wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji
mkoani humo.Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius
Kahyarara akitoa salamu za NSSF wakati wa sherehe za uzinduzi wa
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika Kanisa Katoliki
Bariadi.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda akisaidiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu
uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakionyesha mwongozo wa
uwekezaji mkoani Simiyu baada ya kuzindua.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka
mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu kwa ajili ya utekelezaji wakati wa
hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili
wa UNDP.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda (katikati) akimkabidhi nakala Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini Awa Dabo ambao ndio
wafadhili wa utafiti wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoani Simiyu.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda (wa pili kushoto) akikabidhi nakala ya mwongozo wa uwekezaji
mkoani Simiyu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii
na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda (wapili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara nakala ya mwongozo
wa uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo huo
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.Mgeni
rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf
Mkenda akiabidhi nakala hizo kwa watendaji wa mkoa wa Simiyu.
Kikundi
cha Kwaya ya Simiyu kikiimba wimbo maalum wa kuhamasisha uwekezaji
mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji
mkoani Simiyu.Kutoka
kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo
(UNDP) nchini ambao ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo, Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Antony Mtaka pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda wakitazama burudani ya
kwaya kutoka mkoani Simiyu kwenye sherehe za uzinduzi huo.Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu katika sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.Pichani
juu na chini ni sehemu ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, Wafanyabiashara,
Wanahabari, Viongozi wa madhehebu ya dini pamoja wawekezaji
waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa
Simiyu.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu.Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ESRF na UNDP.Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji wa mkoa wa Simiyu.Meza kuu katika picha ya pamoja na madiwani wa mkoa wa Simiyu.Meza kuu katika picha ya pamoja na kwaya ya mkoa wa Simiyu.Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Simiyu.Meza kuu katika picha ya pamoja na waandishi wa habari.Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,, Awa
Dabo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti
wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya kumalizika
sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu.