Kikosi cha Vinara wa
Ligi Kuu ya Ufaransa timu ya Monaco imeitoa nje klabu ya Man City kwa
jumla ya magoli 3-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa na kutinga hatua
ya robo Fainali.
Ushindi wa Monaco
unafanya mabao kuwa sare ya 6-6, lakini mabao ya ugenini yanaibeba
Monaco ambayo ilifungwa 5-3 jijini Manchester katika mechi ya kwanza.
Monaco walipata mabao mawili ya haraka katika kipindi cha kwanza kupitia Mbappe Lottin na Fabinho, yakadumu hadi mapumziko.
Kipindi cha Leroy
Sane aliamsha matumaini ya Man City kwa kufunga bao katika dakika ya 71
katika dakika ya 77, Tiomoue Bakayoko akayazima kwa kufunga bao la tatu
kwa Monaco ambayo imesonga mbele na kumuacha Kocha Pep Guardiola wa Man
City na majonzi rundo.
VIKOSI
Monaco: Subasic, Sidibe, Raggi, Jemerson, Mendy, Fabinho, Bakayoko, Lemar, Bernardo Silva, Germain, Mbappe-Lottin.
Subs: De Sanctis, Jorge, Dirar, Joao Moutinho, Irvin Cardona, Irvin Cardona, Diallo, Toure.
Subs: De Sanctis, Jorge, Dirar, Joao Moutinho, Irvin Cardona, Irvin Cardona, Diallo, Toure.
Man City: Caballero, Sagna, Stones, Clichy, Kolarov, Sane, Fernandinho, Silva, De Bruyne, Aguero, Sterling.
Subs: Bravo, Zabaleta, Jesus Navas, Delph, Otamendi, Toure, Iheanacho.
Subs: Bravo, Zabaleta, Jesus Navas, Delph, Otamendi, Toure, Iheanacho.
Referee: Gianluca Rocchi (Italy)
Tags
MICHEZO KIMATAIFA