JUMLA ya watumishi wa umma 2,059
wamekwisharipoti Dodoma katika awamu ya kwanza ikiwa ni utekelezaji wa
ahadi ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati
akikabidhiwa uenyekiti wa CCM, Julai 22, mwaka jana.
Awamu ya kwanza ya Serikali
kuhamia Makao Makuu Dodoma inajumuisha Mawaziri na Manaibu wao, Makatibu
Wakuu na manaibu wao, baadhi ya wakurugenzi pamoja na wasaidizi
wachache.
Hayo yamebainika leo (Ijumaa,
Machi 3, 2017) katika Kikao cha Kazi cha Mawaziri na Naibu Mawaziri
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma chini ya
uwenyekiti wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu
aliwataka Mawaziri wote watoe taarifa za idadi ya watumishi wao
waliohamia Dodoma hadi sasa, wamepanga kufanya zoezi hilo kwa awamu
ngapi na lini watakamilisha zoezi hilo. Pia Mawaziri hao walitakiwa
kueleza mahali zilipo ofisi zao kwani amepanga kuwatembelea na
kuzungumza na watumishi.
Wakiwasilisha taarifa hizo,
Mawaziri hao wote wamethibitisha kwamba tayari ofisi zao na wao wenyewe
wameshahamia Makao Makuu Dodoma pamoja na watumishi wao wote walioko
kwenye awamu ya kwanza na wameahidi kukamilisha kuhamisha waliosalia
katika awamu nne hadi sita kulingana na ratiba ya Serikali.
Aidha, Waziri Mkuu amesema baada
ya Serikali kukamilisha ratiba ya kuhamia Makao Makuu Dodoma, Jiji la
Dar es Salaam litabakia kuwa Jiji la kibiashara na wamepanga kuendelea
kuendelea kuliboresha ili shughuli hizo zifanyike kwa ufanisi zaidi.
Mapema, akizungumza na waandishi
wa habari wakati akifungua kikao hicho, Waziri Mkuu alisema kati ya
Julai 2016 na Januari 2017, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya
iliwakamata watu 11,303 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na uzalishaji,
usambazaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema kati ya hao, watu 9,811,
walikutwa na kesi za kujibu ambapo 9,174 wametiwa hatiani, 238
hawakukutwa na hatia na wengine 478 upelelezi wa kesi zao unaendelea.
Pia alisema tangu Tume mpya iundwe Februari mwaka huu, jumla ya
watuhumiwa 79 wametiwa mbaroni na uchunguzi wa kesi zao unaendelea.
“Wengi kati ya hao, wameshikwa na
vithibitisho, ingawa uchunguzi wa kesi zao bado unaendelea. Na hawa ni
wale waliokamatwa na dawa za viwandani kama heroine na cocaine.
Hatujawaingiza wale waliokamatwa na mirungi au bangi. Bado mikoa
inaendelea na kazi, na hii operesheni ni ya nchi nzima,” alisema.
Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma
ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake
ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa
chama cha TANU.
Tangu wakati huo Serikali zote
ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundombinu na hata
awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo.
Serikali ya awamu ya tano iliamua kuhamia Dodoma baada ya kuridhishwa na ujenzi w
Tags
HABARI KITAIFA