Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Aggrey
Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Tabora,Aggrey Mwanri.
Baadhi ya wadau wa zao la tumbaku
wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim majaliwa wakati alipozungumza nao
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi, 16, 2017.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel
Mukandara (katikati) na Makamu wake, Msafiri Ngassa wakiongozwa na
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamis Issah (kulia) kuelekea
kwenye gari la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa
wakamatwe na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao
utakapokamilika. Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.
Mwenyekiti wa WETCU, Gabriel
Mukandara na Makamu wake, Msafiri Ngassa (kushoto) wakiwa kwenye gari
la polisi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza kuwa wakamatwe
na kuwekwa ndani hadi uchunguzi kuhusu utendaji wao utakapokamilika.
Majaliwa alikuwa akizungumza na Wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Machi 16, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora kuwakamata viongozi
wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga
ofisi za chama hicho hadi uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za
chama hicho utakapokamilika.
Pia Waziri Mkuu amevunja Bodi ya
WETCU pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania – TTB kwa sababu ya
kushindwa kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za
umma.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo
leo jioni (Alhamisi Machi 16, 2017) katika kikao kilichofanyika kwenye
ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa
Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita
Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.
Viongozi wa WETCU ambao Waziri
Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu
Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu. Pia
amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi
uchunguzi utakapokamilika.
“Kuanzia sasa watumishi wote wa
kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na
Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi
hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi itakapokamilisha
kazi yake,” amesisitiza.
Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu
wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija kwa sababu ya usimamizi
mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya Tumbaku Tanzania jambo ambalo
Serikali haiwezi kulivumilia.
Amesema “Hatuwezi kuwa na ushirika
ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea sh. bilioni 15 ambazo
walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia waliwalipa wazabuni sh, bilioni
10 ambazo hawajazikatia risiti,”.
“Wakati wanachama ambao ni
wakulima wakiendelea kutesema WETCU walinunua gari la sh. milioni 269
kinyume na na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau ambao ulipitisha
zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa chama
hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana
na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa
tumbaku kukosa tija.
Amesema WETCU kimekithiri kwa
matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano suala la ukarabati wa
ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa ikarabatiwe kwa sh.
milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za Tabora na Urambo
zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na hazikukarabatiwa.
Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku
ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wkatiikiwa inazalishwa hap nchini.
Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya kwa dola katika sekta ya tumbaku
na badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho
kimekuwa kiwanyonya wakulima.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, wakuu wa
wilaya zote za mkoa huo pamoja na Maofisa Kilimo na Ushirika kuhakikisha
wanasimamia vizuri zao hili ili liweze kuwa na tija kwa wakulima na
Taifa kwa ujumla.
Pia amewaagiza Maofisa Kilimo
waende vijijini na kuwatambua wakulima wa tumbaku katika kila kijiji na
kuwasajili. “ Kuanzia leo Maofisa Ushirika wabadilishe mienendo ya kazi
nataka wasimamie zao la tumbaku kwa umakini zaidi.”
Tags
TABORA TUMBAKU