Vinara wa Ligi Kuu nchini
Uingereza timu ya Chelsea imepunguzwa kasi katika kuwania ubingwa baada
ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Crystal Palace kwenye uwanja
wao wa nyumbani.
Chelsea walikuwa wa kwanza kupata
bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji Ces Fabregas dakiak ya 5 akipokea
pasi nzuri toka kwa Harzad hadi hivyo Palace waliweza kusawazisha
kupitia Wilfred Zaha dakika ya 9.
Christian Benteke alishindilia
msuli wa pili dakika ya 11 na kuweza kuwalaza mapema vijana wa Conte
hadi Mpira unamalizika Chelsea wamelala 2-1 na kupunguzwa kwa alama 7 na
Tottenham ambao wameshinda na kuweza kufikisha alama 62 huku Chelsea
akibaki na Alama 69.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA