Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga imerudi kwenye mbio za ubingwa baada
ya kulipa kisasi kwa Azam FC cha bao 1-0 mchezo uliochezwa kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga wakicheza bila ya nyota wake
watano ambao ni Yondani,Kessy,Kamusoko,Tambwe na Ngoma huku Azam
ikiwakosa Agrey,Kapombe na Bocco timu hizo zilianza kushambuliana
kipindi cha kwanza huku Wana rambaramba wakionekana kuutawala Mchezo na
kukosa nafasi nyingi za wasi.
Yanga imeendelea kupata rundo la
majeruhi baada ya kiungo mkabaji wao Justine Zulu kuumia kwa mguu wa
kushoto na kupelekea kukimbizwa Hospitali dakika ya 30 kwa kuchezewa
madhambi na Himid Mao wakati akijiandaa kupiga Mpira katika eneo la Azam
na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin.
Azam FC waliendelea kulishambulia
lango la Yanga huku wachezaji wake kukosa umakini wa kumalizia nafasi
ambazo walizipata na dakika ya 43 Mshambuliaji wa Azam Yahya Mohammed
aliumia kwa kubanwa na msuli hivyo kushindwa kuendelea na nafasi yake
kuchukuliwa na Mghana mwenzake Samuel Afful hadi mapumziko timu zilikuwa
nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote kufanya mabadiliko na kuanza kushambuliana kwa zamu huku Yanga
wakiingia kwa kucheza kimbinu zaidi kwa lengo la kupata pointi tatu
Muhimu na katika dakika ya 70 Mzambia Obrey Chirwa aliwanyanyua
mashabiki wa wake pamoja na benchi la ufundi baada ya kumtoka beki wa
Azam FC, Yakubu Mohamed kufuatia pasi ndefu ya kiungo mchezeshaji,
Haruna Niyonzima.
Kwa Matokeo hayo Yanga imeongoza Ligi kwa muda baada ya kufikisha jumla ya pointi 56 na nafasi ya pili ikishikwa na mahasimu wao Simba wenye pointi 55 na kesho watashuka dimbani kucheza na Kagera Sugar Mjini Bukoba na kuendelea kufukuzana kwenye mbio za Ubingwa.

Baada ya Mpira kumalizika
FULLSHANGWEBLOG.COM ilifuatilia ili kujua hali ya Justine Zulu ambaye
alikimbizwa Hospital na kupata taarifa kuwa Mchezaji huyu ameshonwa
nyuzi tisa kwenye Mguu wake na kuweza kuongeza idadi ya majeruhi katika
kikosi cha Yanga ambacho kinajiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho
dhidi ya MC Alger mwishoni mwa wiki inayokuja
Vikosi Yanga ; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul,
Mwinyi Mngwali, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma
‘Makapu’, Simon Msuva/Juma Mahadhi , Justin Zulu/Emmanuel Martin , Obrey
Chirwa, Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya na Haruna Niyonzima.
Azam; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Yahya Mohmmed/Samuel Afful , Shaaban Iddi/Bruce Kangwa na Ramadhani Singano ‘Messi’/Joseph Mahundi .