Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi amesemacheti cha kuzaliwa kunamuwezesha
mtoto/mtanzania kupata haki za msingi kama raia.
Prof Kabudi amesema hayo mjini
Dodoma wakati akifungua semina ya wadau kujadili mapitio ya sheria
zinazohusiana na usajili wa matukio muhimu ya binadamu nchini.
Amesema ni muhimu kuimarisha
harakati za kukuza mwamko wa usajili wa watoto na watanzania kwa ujumla
wanapaswa kusajiliwa na kupata vyeti kwani kuwa na vyeti hivyo
kutawawezesha kupoata haki zao za msingi .
Amezitaja haki hizo kuwa ni
pamoja na kuwa na jina,kupata kazi, kutambulika kama raia, na kuzuia
watoto chini ya miaka 18 kuingizwa katika vita, ajira za utroto na hata
kushtakiwa kwa makosa ya jinai na kuwekwa rumande na watu wazima.
Prof Kabudi alichukua nafasi hiyo
kuihakikisha timu hiyo kwamba atahakikisha sheria hiyo ya usajili wa
vizazi, vifo na talaka inafanyiwa marekebisho haraka ili ziweze kwenda
na wakati uliopo sasa na hivyo kukuza usajili wa watanzania .
‘Nitahakikisha sheria hii
inafanyiowa marekebisho haraka, kwani kuirekebisha sheria hii kutaifanya
iendane na wakati na kufanya usajili wa watanzania kuongezeka, hatuna
budi kuongeza bidii katika kazi hii ili watanzania wote waweze
kusajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa,” alisema Prof. Kabudi.
Awali akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri Kabudi Mweyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria
nchini Jaji Aloysis Mujuluzi tume yake iliendeesha utafiti juu ya sheria
hiyo ya usajili katika mikoa 13 nchini na kuunganisha na tafiti za
sheria mbalimbali ili kuhakikisha maboresho ya sheria hiyo yanazingatia
maoni ya wadau mbalimbali nchini.
Alisema wanaifanya kazi hiyo kwa
moyo mmoja na watakapoikamilisha tu watamkabidhi Waziri Kabudi ili nae
atoe maoni yake kama mdau ili kuweza kuwa na sheria mpya itakayokidhi
mahitaji ya wakati uliopo na wakati ujao.
Alisema katika tafiti yao
wamegundua kuwa mfumo wa usajili wa raia nchini haujakaa vizuri kwani
mifumo hiyo haiuzungumzi lugha moja na hivyo kuwachanganya watanzania.
Aliitaja mifumo hiyo kuwa ni Vitambulisho vya Taifa, kadi ya mpiga kura ,
hati ya u
Kusafiria na cheti cha kuzaliwa
Alisema umefika wakati sasa kwa
mifumo hiyo kuzungumza lugha moja na kuongeza kuwa mifumo yote hiyo
ilitakiwa itegemee chetio cha kuzaliwa cha mtu na ndipo waendelee na
utaratibu wake.
Alisema kutokana na hali hiyo ndio maana watanzania wachache wapatao asilimia 13.4 tu ndio wenye vyeti vya kuzaliwa
Tags
CHETI CHA KUZALIWA