BANDA MEDIA BLOG

HIVI NDIVYO SHIRIKA LA KIMATAIFA GIRL GUIDES...... LILIVYOZINDUA UPANDAJI MITI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MTUMBA MANISPAA YA DODOMA

Wafanyakazi wa shirika hilo wakichimba mashimo tayari kwa kupanda miti katika shule ya msingi Mtumba
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa na Michi ya miti ya vimvuli na matunda kabla ya zoezi la upandaji kuanza
Wanafunzi wakiendelea na uchimbaji wa mashimo
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo KATIBU tawara msaidizi Aziza Mumba  akiweka mbolea katika mti aliupanda shuleni hapo
Mwenyekiti wa Taifa wa Shirika la Girl Guides Martha Qorro akimwagilia mche wa mti alioupanda katika shule ya msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo lililojumuisha mti ya matunda na vimvuli 600 toka shirika hilo [PICHA NA JOHN BANDA WA BANDA BLOG]
























PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA MKOA WA DODOMA WALIOSIMAMA NYUMA

John Banda, Dodoma
SHIRIKA la Tanzania Girl Guides  Association limezindua mradi wa upandaji miti katika shule ya msingi ya Mtumba manispaa ya Dodoma huku likiwa na lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akiongea katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Girl Guides nchini Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshanza upandaji wa miti hiyo katika mkoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza
Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.
Nae Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Gaides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawara msaidizi Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika la Girl Guides zinafaaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye lutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG