1. Kwanza mdomo wa mbu haupo kama sindano za kawaida zinazotumika, mlija
wa mbu ambao hutumika kuingizia mate yenye vimelea vya malaria ni
tofauti na ule unaotumika kufyonza damu kutoka kwabinadamu, kutokana na hili kwaiyo damu tu ndio huingia kwenye mwili wa
mbu kutoka kwa binadamu alieng`atwa na mbu, na mate tu ya mbu ndio
huingizwa kwenye mwili wa binadamu.
2. Pili magonjwa yote ambayo huambukizwa na insekta kama, matende na
malaria aya magonjwa yanaweza kusambazwa na mbu kwa sababu vimelea vya
aya magonjwa huweza kujizalisha(multiply) katika mwili wa mbu, ambapo
hivi vimelea huweza kusambaa hadi kwenye mate ya mbu baada ya hapo
huweza kuingizwa kwa kung`atwa binadamu. Tofauti ni kwamba vimelea yani
virusi vya ukimwi(vvu) vinapoingia kwenye mfumo mzima wa mmeng`enyo wa
mbu humeng`enywa kama chakula cha kawaida kisha hutoka kama uchafu, ili
virusi vya ukimwi viweze kujizalisha(multiply) ni lazima viingie kwenye
seli maalumu za binadamu.
3. Tatu, virusi vinavyosabisha ukimwi huzunguka taratibu kwenye damu
ukilingansha na vimelea vinavyosababisha magonjwa yatokanayo na
insekta(mbu), hii inamaanisha ata mbu anaponyonya damu kwa binadamu
ambaye tayari virusi vya ukimwi hawezi kunyonya idadi kubwa ya virusi.
Tafiti zaidi zinaonyesha kwamba ili mbu aweze kueneza virusi vya ukimwi
kwa binadamu mtu huyo ina bidi ang`atwe na mbu million kumi(10) idadi
hii ya mbu ndio inaweza kutengeneza uniti moja(1) ya kirusi apo ndipo
huenda kikasababisha kueneza vvu, hii inamaanisha ata ikatokea kwa
bahati mbaya uka mmeza mbu aliye mng`ata binadamu ambaye ana virusi
vinavyosabisha ukimwi huwezi kupata maambukizi.
UHIMU
Achana na ngono zembe kwani
huchangia kwa asilimia kubwa maambukizi
ya VVU ambavyo usababisha UKIMWI…
