Na Shamimu Nyaki WHUSM
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo pamoja na Wizara ya Habari,Utalii Utamaduni na Michezo ya
Zanzibar zimekubaliana kushirikiana katika Michezo ikiwa ni mikakati ya
kuleta mafanikio ya soka ndani na nje ya nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa lengo la kukutana na Waziri
mwenye Dhamana ya Michezo visiwani Zanzibar ni kutimiza lengo la muda
mrefu la kukutana na kupanga mikakati mbalimbali ya kuinua soka la nchi
hizo.
“Tumekutana kuweka mikakati imara
ya kutimiza lengo la muda mrefu la kutafuta na njia mbalimbali
zitakazosaidia soka letu kukua na kuimarika ndani na nje ya ya nchi
zetu”,Alisema Dkt.Mwakyembe.
Aidha ameipongeza Zanzibar kwa
kufanikiwa kuwa mwanachama halali wa Shirikisho la mpira wa miguu barani
Afrika(CAF) na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika maendeleo
ya soka ya nchi hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Habari
Utalii Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Mhe.Rashidi Waziri amesema kuwa
Wizara yake ina jukumu kubwa kuendeleza Soka la Zanzibar hasa katika
kipindi hiki amabacho imepata nafasi katika Shirikisho la mpira wa miguu
la Afrika.
Mhe. Waziri Rashidi ameongeza kuwa
ushirikiano wa Kisoka baina ya Wizara hizo utaleta hamasa kwa
wawekezaji wa soka kupata uwanja mpana wa uwekezaji kwa Tanzania Bara na
Zanzibar.
“Tanzania ina matarajio makubwa
sana kwakuwa kwa kipindi kirefu tumekuwa wasindikizaji hivyo ushirikiano
ni njia pekee ya kuweza kutatua changamoto ya kuingia katika soka la
FIFA”
Tags
BARA NA ZNZ KISOKA