
Ni wakati wa matazimio mapya. Miongoni mwa maazimio(resolutions)
zinazoongoza ni pamoja na ile ya kuishi maisha yaliyo na afya bora zaidi
na
furaha. Afya na furaha ni mambo mawili makubwa sana katika maisha
yetu.Ukichunguza sana takribani kila kitu tunachokifanya ni katika
mpambano wa kimaisha wa kuwa na afya bora zaidi na kuwa na furaha.
Sote tunakubaliana kwamba afya bora ndio kila kitu.Ukiwa tajiri
kupindukia halafu ukawa na afya mgogoro,ni wazi kwamba huwezi
kuzifurahia hizo hela zako.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya bora katika maisha,
.Lakini kabla sijaendelea mbele sana,naomba niweke wazi kwamba afya bora
haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake bali pia fikra
chanya(positive
attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba siku zote unakuwa na
mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na watu wenye mawazo chanya.
1.Kunywa Maji kwa wingi-
Bila shaka unakumbuka msemo “Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa.Maji ni
uhai sio tu kwa mazingira yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au
miili yetu.Maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu.Asilimia 60% ya miili
yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya
kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini.Maji ndio hubeba
virutubisho na oxygen.
Kiasi cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama
vile unyevu(humidity) wa mahali ulipo,shughuli zinazohusisha mwili
anazozifanya mtu na
pia uzito wa mwili.Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji.Vyakula tunavyokula
huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu.Kwa hiyo
tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za
maji kwa siku.
Njia rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika
kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi(colorless) au
kuwa wa njano kidogo.Kinyume cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya
kutosha mwilini.Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na
midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.
2.Pata Usingizi wa Kutosha:
Unakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende
tukalale mapema ili tukue? Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi
ni sehemu muhimu sana katika afya.
Ukiachilia mbali faida za usingizi kwa ajili ya afya za akili/ubongo
wetu,usingizi au mapumziko ya kutosha ni muhimu kwa miili.Afya njema
huenda sambamba na mapumziko.Ni wakati wa kuupa mwili nafasi ya
kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha kwamba tunakuwa
na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka mapema.
3.Fanya Mazoezi-
Hili linaweza kupita bila maelezo ya ziada.Mazoezi ni muhimu sana kwa
afya bora. Fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki.Jipatie muda wa
kutembea japo kwa dakika 30. Kama inawezekana nenda Gym.Badala ya
kupanda lifti pale kazini kwako au mitaani,tumia ngazi za kawaida.Egesha
gari lako mbali kidogo na unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk.
Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi
hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa
mbalimbali,kupunguza unene(bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio
afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)
4.Kula Matunda Kwa Wingi
-Matunda ni chanzo kizuri sana cha madini na vitamins ambazo miili yetu
inahitaji sana kwa ajili ya afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa
mfano, yana faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C
unavyobugia kila leo? Aina mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi
vingi zaidi kiafya ni
Parachichi(Avocado),apple,matikitimaji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit),Kiwi,Guava,mapapai,machungwa,
strawberries nk.
5.Kula mboga za majani
Kama ilivyo kwa matunda,mboga za majani(vegetables) ni muhimu sana kwa
afya zetu. Wataalamu wa afya wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za
mboga za majani na matunda.Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za
mboga za majani na matunda.
6.Punguza Kula Vyakula vya Makopo
Kutokana na jinsi dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa
muda wa kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye
makopo ambavyo ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi
kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya
makopo huwa na ingredients ambazo hazifai kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi
miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo
cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia
kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo havina sukari
au chumvi.
7.Jipende
Kama nilivyodokeza hapo mwanzo,afya bora huenda sambamba na afya ya
akili/ubongo.Njia mojawapo ya kupata afya hiyo ni pamoja na
kujipenda.Pengine unajiuliza,kuna mtu ambaye hajipendi? Ukweli ni kwamba
pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye hajipendi.Tofauti inakuja
pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume kabisa na mapenzi ya mwili.
Mfano,uvutaji sigara,unywaji pombe kupindukia,kutojisafisha mwili wako
kwa mfano kuoga,kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia
ambazo zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.Kama unaupenda utautumia vibaya au kuuharibu?