Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),
Valentino Mlowola amesema wakati anateuliwa na Rais John Magufuli
alikuwa nchini Uganda kutoa ushahidi katika kesi ya ugaidi inayomkabili
mtu aliyemkamata hapa nchini kwa tuhuma za mauaji ya watu 76 nchini
humo.
Amesema kwamba, mtuhumiwa aliyekuwa akitoa ushahidi dhidi yake anadaiwa
kuua watu 76 nchini Uganda waliokuwa wakiangalia michezo ya Kombe la
Dunia kupitia televisheni.
“Hata wakati napewa taarifa ya kuja kuongoza chombo hiki nilikuwa
mahakamani natoa ushahidi wa kesi ambayo Waganda 76 waliuawa katika
shambulio wakati wa World Cup (mashindano ya kombe la dunia), kwa sababu
mtuhumiwa aliyepeleka mabomu Uganda alikuwa Mtanzania.
Tags
Uganda
