Na kwa kuwa walisema yeye JK ni Rais dhaifu, asiyechukua hatua,
anayewachekea n.k..ndipo sasa akatuletea CHUMA!....I mean "CHUMA
kilichopo hapa Ikulu ya MAGOGONI muda huu,...Mirija imezibwa...Vibaka
wameshikwa Koromeo...Wauza Unga wanasaga meno....Chuma kinanyoosha
nchi!..wanapiga kelele kama ndama!.
JK wakati anaondoka alisema wazi "Mimi naondoka, mlisema mimi mpole,
sasa nimeleta Chuma hiki"...na kana kwamba haitoshi akasema "Kila zama
na kitabu chake"...akaondoka zake...Chuma kikaingia kazini.
Siku ya kwanza Kazini JPM akaanza na Management by Walking Around
(MBWA)..akashusha Mbwa wakali kunusa Wizara ya Fedha....watu wakasema
"anaigiza huyo!"...sasa leo 2017 igizo limekuwa Isidingo?..Mbona
mnabweka?....mtulie "Bado"
Watu wakapinga hata ununuzi wa ndege kufufua ATC,.ndege zikaja wakaita
"Pangaboi" akiwemo zitto ambaye akasisitiza ni "Reject"
hazifai!...Wakaenda mbali kwa kusambaza picha za ndege za zamani
zilizoanguka kwamba Raia watishike wasipande..lengo likaferi..halafu hao
hao wanahoji eti oo hizi bilioni 8 kwa hizi ndege mbili tunaomba
mchanganuo wake !...Vituko!
Wapo wanaocheka sera ya Viwanda...kwamba wanauliza viwanda viko wapi
kana kwamba Viwanda ni Vyandarua vya UNICEF unasambaza...thats Means hii
inaonyesha namna gani watu hawataki fedha zielekezwe kwenye miradi
itakayogusa future Generation, yaani kiwanda kitakachozinduliwa 2021
hawataki...Fly Overs zitakazozinduliwa 2018 hawataki...Kiwanda cha nguo
kitakachokamilika 2018 hawataki ...madaraja hawataki...wanataka vitu
vianguke kama mabibo juu ya mkorosho...kwamba Viwanda wanaita
''Vi-Wonder"..just hitting their own backbones...who cares?
Most of Wanahabari wamekuwa mateja wa udaku, wanasema Uhuru
unaminywa...Uhuru wa Manyani..hivi kuna mtu kawakata kuandika"MADAWA YA
KULEVYA NI HATARI"on front page?..kutwa ni ku-attack personality za watu
kuliko maslahi ya taifa...hawa nao wanamkumbuka JK ambaye walijisikia
huru kumuandika kwa namna wanayotaka na wengine bila staha na
Adabu....halafu njaa yao nayo inawafanya wanatofautiana misimamo!..leo
wanasema Papai..kesho Tango...hii ni ishara ya kwamba kuna influence
nyuma yao..tena inayohitaji TAKUKURU!
Tags
RAIS MAGUFULI
