
Pamoja na hayo, Marcon ambaye ameoa mke mwenye umri wa miaka 64 ,ana
mambo mengi ya kufurahisha na kuvutia maishani mwake hususan kuhusiana
na mkewe huyo ambaye anamzidi umri kwa kiasi cha miaka zaidi ya 24.
Mkewe huyo alikuwa ni mwalimu wake wa darasa miaka ipatayo 24 iliyopita
ambapo mwalimu wake wa darasa wakati huo alikuwa na binti ambaye alikuwa
mwanafunzi mwenzake darasa moja. Wakati huo, kila mtu, wakiwemo wazazi
wake Marcon, walifikiri binti huyo wa mwalimu alikuwa rafiki yake,
wakati hawakuwa hivyo.
Katika mlolongo huo wa vituko, Marcon alijikuta katika mapenzi na
mwalimu wake wakati yeye akiwa na umri wa miaka 15 ambapo wakati huo,
mwalimu huyo alikuwa ameolewa akiishi kwa furaha na akiwa na watoto
watatu
Alipofikisha umri wa miaka 17, aliamua kumuoa mwalimu huyo, wakati huo akiwa na umri wa miaka 42.
apendanao hao walifunga pingu za upendo mwaka 2007 wakati huo ‘mlume’
huyo akiwa na umri wa miaka 30 na ‘mrembo’ wake akiwa anapiga hodi
katika umri wa miaka 55.
Mwanandoa huyo wa kiume anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ufaransa
mwezi ujao akiwa amebakiza miezi sita kufikisha umri wa miaka 40 wakati
ambapo kipenzi chake, yaani mkewe, ana watoto (watu wazima) watatu na
wajukuu saba sasa.
Ni vyema pia kufahamu kwamba mtoto wa kwanza wa mkewe huyo anamzidi
Marcon kwa umri wa miaka miwili, wakati ambapo mtoto wake wa pili,
aliyekuwa kipenzi na mwanafunzi mwenzake na Marcon wakiwa darasa moja,
wanalingana umri.
Tags
UFARANSA