Jana Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amekiri kupokea
taarifa za katazo lililotolewa na serikali ya Kenya juu ya uuzwaji wa
gesi zinazotumika majumbani zinazotoka Tanzania na kusema wataalamu wa
wizara wanazifanyia kazi taarifa hizo.
Waziri Mwijage ametoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na mwandishi
wahabari wa Azam Two mjini Dodoma baada ya kuzagaa kwa taarifa za
serikali ya kenya kupiga marufuku ya gesi zamajumbani za Tanzania kuuzwa
Kenya na kukiri kuwa Kenya wamekuwa na chokochoko kadhaa lakini
watahakikisha wanakaa chini kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha viongozi wa juu wa nchi hizi mbili.
Tags
mwijage