Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Nchini Dr. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko makubwa ya Viongozi
wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwateua Wakuu
Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa iliyopo Tanzania Bara
na Visiwani Zanzibar.
Katika Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus
Faustine Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa
mkoa wa Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Selemani Bandiho Kameya amehamishiwa Mkoa wa
Tabora.
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Paulus Achacha amehamishiwa
Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara Naibu
Kamishna Peter Jerome Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi
ya Kamishna Msaidizi Ali Mohamed ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji mkoa wa Arusha.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Mkemi Mhina Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini
Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Muhsin Abdallah Muhsin ameteuliwa
kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mjini Magharibi na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja.
Katika mabadiliko hayo baadhi ya
Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa wamebaki katika Vituo vyao vya kazi vya awali
akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna
wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Laurent Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Alexander Ihano na Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Fredrick Eustace Kiondo.
Wengine waliobaki kwenye vituo
vyao vya awali ni pamoja na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Abdallah
Ramadhani Towo mkoa wa Kagera na Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Anastazia Gasper Ngatunga mkoa wa Shinyanga.
Katika mabadiliko hayo Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Dr. Makakala pia amewateua Viongozi wa Uhamiaji wa
Mikoa wapya katika baadhi ya mikoa hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Mary Francis Palmer kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es
Salaam, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Plasid Mazengo, Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji James Andrew Mwanjotile,
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope
Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, na Kamishna Msaidizi
wa Uhamiaji Hosea Alphonce Kagimbo Mkoa wa Njombe.
Wengine ni Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Rashid Salum Magetta Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Carlos John Haule, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Julieth Deodatus Sagamiko Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Joseph
Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro na Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Paul Laurent Eranga, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza.
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin
Crispin Ngonyani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga,
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Shaban Omar Hatibu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Katavi, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Remigius Ibrahimu Pesambili
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji
Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.
Aidha Mrakibu Mwandamizi wa
Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji
cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume [AAKIA] na
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Fulgence Andrew Mutarasha
kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius
Nyerere[JNIA].
Imetolewa na
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini
Dr. A. P. Makakala
3 Machi 2017
Tags
UHAMIAJI