Msanii Nay wa Mitego ambaye mwisho wa wiki amekutana na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amefunguka na
kushukuru kukutana na Waziri mwenye dhamana na kusema kwa sasa hakuna
anachoweza kubadilisha kwenye wimbo huo.
Nay wa Mitego anasema kwa sasa hakuna kitu anachoweza kubadilisha kwenye
wimbo huo kwani haukuwa na lengo baya ila lengo lake lilikuwa ni
kufikisha ujumbe ambao tayari anasema anaona umeanza kufika, sehemu
husika.
Nay wa Mitego anasema mapendekezo ambayo aliyatoa Mhe. Rais John Pombe Magufuli atayafanyia kazi.
Tags
NEY WA MITEGO
