Baada ya ukimya wa miaka kadhaa na misukosuko aliyopitia, Ray C ameweka
wazi mpango wake wa kuyateka tena mawimbi ya radio na vituo vya runinga
kwa kuachia mzigo wenye ujazo kamili.
Mwimbaji huyo ambaye tangu mwaka jana alikuwa akipost picha kadhaa
kwenye mitandao ya kijamii akiwa studio, amefunguka kupitia Twenzetu ya
100.5 Times Fm kuwa tayari ameshapika nyimbo nane ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya albam yake.
Hata hivyo, Ray C amedai kuwa hajaridhika na nyimbo zote alizofanya
hivyo ataendelea kurekodi kabla ya kuanza kurusha makombora mfululizo
yakifuatiwa na albam hiyo.
“Hata hivyo bado sijaridhika ni nyimbo gani nitoe kwa sababu bado
nilizokuwa nazo sijaridhika kwa sababu nimekulia katika maisha ya kutoa
nyimbo kumi au kumi na tano halafu ndio natoa wimbo mmoja [kwanza],
sijazoea kurekodi wimbo mmoja halafu nikaharakisha kutoa,” alisema Ray
C.
Aliongeza kuwa anachofanya ni kuhakikisha anapata nyimbo tano bora zaidi
zitakazochuana kila atakapokuwa akiziachia na kwamba kila siku
anapoingia studio hujikuta akirekodi wimbo mkali zaidi ya uliopita, ndio
sababu ya kutaka kuongeza nyingine.
‘Kiuno Bila Mfupa’ alidai kuwa anatarajia kuiza albam yake na kuiuza duniani kote kupitia mtandao.
Hivi karibuni, Ray C aliwaonjesha mashabiki wake ladha ya sauti yake kwa
kurudia wimbo wa Recho ‘Upepo’ na kudhihirisha kuwa bado ana uwezo
mkubwa.
Tags
Ray C
