Dola Indidis ni mwanasheria kutoka Kenya aliyeishtaki Israel kwa kumuua
Yesu). nadai hakuipeleka kesi mahakamani kwa misingi ya kidini bali kwa
misingi ya Kisheria. Anasema "Its academic thing not a theological
thing" Yeye anachoangalia si unabii bali legal procedure.
Pia amesisitiza ameamua kumtetea Yesu kama mtoto wa Yusufu (fundi
seremala) na sio Yesu kama Masihi "I look Jesus as son of Joseph not as
the Messiah"
Alipoulizwa mbona ilitabiriwa Yesu atakufa, anasema anafahamu hilo ila
hoja sio Yesu kufa, hoja yake ni process iliyotumika kumuua haikuwa sawa
kisheria. Anadai mahakama ilikosea kujiingiza kwenye kesi hiyo "The
court should not involve itself in that crooked case."
Anasema Yesu ungehukumiwa kifo kwa kufuata taratibu za kisheria
kusingekuwa na shida, ila aliuawa kikatili bila kupewa haki ya
kusikilizwa. Wakati Yesu anpelekwa mahakamani (kwa Pilato) tayari
alishaanza kusulubiwa kabla hata hukumu haijatoka.
Huo ulikuwa ukiukwaji wa sheria maana mtuhumiwa hawezi kuadhibiwa kabla
ya mahakama kujiridhisha kuwa mtu ana hatia. "no punishment could be
made unless the court proved beyond the reasonable doubts that Jesus was
guilt" Anasema Yesu angepata wakili wa kumtetea angeachiwa huru. Hata
kama ilimpasa kufa angeuawa kwa namna nyingine.
Anadai pia Pilato hakuwa na nguvu ya kisheria ya kusikiliza ile kesi na
hata yeye alikiri hilo ndio maana akawarudisha wayahudi kwa Herode.
Lakini akalazimishwa kutoa hukumu kwa pressure ya mfalme Herode. "Pilate
had no jurisdiction to give the judgment, he confessed, and also he
confessed the innocence of Jesus"
Pia anadai Pilato alikiri Yesu kutokuwa na hatia, lakini bado
alisulubiwa. Sasa kama Pilato ndio alikuwa Jaji na hakuona hatia ya Yesu
kwanini bado Wayahudi walimsubisha?
Akaongeza kuwa kitendo cha Wayahudi kumsulubisha Yesu mbele ya Jaji
(Pilato) ni kujichukulia sheria mkononi na ni uvunjifu wa haki za
binadamu. "Jesus was tochered in-front of Judge, that is abuse of Human
rights"
Anadai misingi ya haki ilikiukwa katika kuongoza kesi (miscarriage of
Justice) na Yesu hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alikuwa
akilalamika. "Even Jesus complained but he was not given right to be
heard,that is mis-courage of justice."
Amesema pia kuwa maamuzi hayakuzingatia principle of natural justice, na
hukumu inapaswa kurekebishwa na Israel kuomba msamaha. "The judgment
was bad in law and should be quashed"
Ametumia kesi ya Mwai Kibaki vs Daniel Arap Moi 1999 kama refference ya
kesi yake (MWAI KIBAKI Vs DANIEL TOROITICH ARAP MOI, Case Number :Civ
App 172 of 1999").
Anaungwa mkono na makanisa kutoka nchi za Norway, Marekani, Israel, Uingereza, Tanzania, Afrika Kusini, Canada na Ujeruman
Tags
yesu
