Muda mfupi sana uliopita nlikutana na jamaa mmoja yuko bandari,
aliyonieleza ndio nimekubali kua Magu kapanyoosha sana bandarini. Pale
bandari ndugu zangu wachaga walipageuza shamba la bibi, jamaa ananiambia
kuwa enzi hizo ilikua inakuja meli nzima na inapita bila kulipiwa hata
kumi, makontena ya magari, electronics n.k yalipitishwa kama makontena
ya mtumba, kifupi kila mtu alikua anajipigia atakavyo.
Jamaa alikua kitengo cha kawaida sana lkn ananiambia amejenga gorofa
huko Bunju, anasema enzi hizo ilikua mtu kurejea nyumbani na laki tano
kwa siku analalamika kua siku ilikua mbaya sana, kifupi huko ndiko
bandari yetu ilikokua imefika, anasema hata kina Kipande wameshinda kesi
maana walipokea vimemo kutoka nyumba adhim vyenye maagizo yakutoa
makontena ya watu, tena wengine sasa wanajitolea sana Serikalini
(wanatakatisha pesa).
Ila sasa jamaa anasema huko bandari ni balaa, ukaguzi wake sio kawaida,
na wanaokagua ni watu hawajulikani wanatoka wapi na ofisi gani, jamaa
anaemiliki gorofa Bunju leo alipanda daladala, kawa mpole na mwenye
nidhamu haswa, na anasema Magu kabana haswa..Kifupi nachukua nafasi
kumpongeza Magu maana kwa ushuhuda huu ni kweli kafanya mengi ambayo
wabaya wake hawapendi kuckia..
Komaa mzee tunyooshe mpaka maji tuyaite mma
