| Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Dkt Allan Kijazi akichangia mada kuhusu uhifadhi wa mto Ruaha mkuu |
![]() |
| Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kulia akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi leo |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akichangia mada juu ya uhifadhi wa mto Ruaha mkuu |
![]() |
| washiriki wa mkutano huo wakitoa maoni yao |
![]() |
| Mbunge wa Mary Mwanjelwa akichangia katika mkutano huo |
![]() |
| Waziri wea Mazingira na muungano January Makamba akipokea maelekezo toka kwa makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo |
![]() |
| Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akichangia jinsi ya kulinda mto Ruaha mkuu |
![]() |
| Waziri wa Maliasili na utalii Dkt Jumanne Maghembe akifafanua jinsi ya kuungana kulinda maji kwa faida ya wananchi na wananya |
![]() |
||
| Mbunge wa Makete Dkt Norman Sigalla Na MatukiodaimaBlog |
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kikosi kazi kilichoundwa na ofisi yake kufanya kazi ya kunusuru mto Ruaha mkuu.
Akizungumza leo wakati wa mkutano
wa kwanza wa kuhifadhi Ikolojia ya mto Ruaha alisema kuwa uwepo wa
kikosi kazi hicho ni kuacha maneno na kuonyesha utendaji.
Alisema lengo la kuunda kikosi
kazi hicho bila kwa sasa kushirikisha sekta binafsi ni kutaka kufagia
nyumba yetu na kuona kasoro zilizojitokeza na baada ya hapo
watashirikisha sekta binafsi.
Kwani alisema ushirikishwaji wa sekta zote ni muhimu kwa ajili yakunusuru mto Ruaha mkuu.
Huku akitaka wanahabari
kushirikiana na kikosi kazi kuandaa vipindi vya elimu ya uhifadhi wa mto
Ruaha mkuu na kuvirusha kwa wananchi.
Hata hivyo alisema kuwa kuwepo kwa
kikosi kazi hicho hausimamishi sheria zilizopo katika uhifadhi wa
mazingira na kutaka wizara zote kuungana kusimamia sheria za usimamizi
bora wa maji.
Alisema kutokana na mgongano
uliopo wa kila wizara kutetea eneo lake serikali imepoteza pesa nyingi
sana katika uhifadhi na hivyo kutaka kuanzia sasa wizara zote kuungana
kunusuru mto Ruaha mkuu.
Aidha alisema anaunga mkono wazo la mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam la kutaka kuangalia pia mito midogo.
Hata hivyo alitaka watumishi wote
wanaoshindwa kutimiza wajibu wao kama mabwana shamba, misitu na wengine
kufanya kazi kulingana na pesa wanazolipwa na kuwa serikali itaweka
usimamizi sahihi kuona kila mmoja analipwa kulingana na kazi.
“Ni imani yangu kuwa kikosi kazi hiki cha kunusuru mto Ruaha kitafanya kazi yake vizuri “
Alisema kuwa Papa Francis alipata kusema kuwa Mungu ukimkosea atakusamehe ukitubu ila mazingira ukiyakosea hayatakusamehe.
Tags
MTO RUAHA MKUU







