Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha tano cha
mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini
Dodoma.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge
katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda , Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika
kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali za
wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Mwibara(CCM) Mhe. Kangi
Lugola akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Fakharia Shomar Khamis (CCM) akiuliza swali katika kikao cha tano cha
mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali
za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi akijibu hoja mbalimbali za
wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mwita Waitara akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na
Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika
kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Urambo (CCM) Magreth
Sitta akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Iringa Mjini
(CHADEMA), Mhe. Peter Msigwa akiuliza swali katika kikao cha tano cha
mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi
Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya akijibu hoja mbalimbali za
wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Shaurimoyo
(CCM), Mattar Ali Salum akiuliza swali katika kikao cha tano cha
mkutano wa saba wa Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira kazi na watu wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama(kushoto) wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa saba wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma katikati ni
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
sanaa na Michezo Mhe. Anastazia wambura(Kushoto) na Naibu Waziri wa
Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya wakifuatilia
kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri
Mkuu Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora Mhe. Angellah Kairuki katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao cha tano cha mkutano wa saba wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Wajumbe nane kutoka Baraza la
Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia shughuli za kikao cha tano cha mkutano
wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
……………….
SERIKALI YAFAFANUA KUSHAMIRI KWA
BIASHARA YA VYUMA CHAKAVU, MPANGO WA KUUNDA BODI MPYA YA TUMBAKU NA
UTENGAJI ASILIMIA MAALUM KWA WANAFUNZI KUTOKA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR
Dodoma,Jumanne, 11 April, 2017.
Serikali imetoa ufafanuzi
kuhusu kushamiri kwa Biashara ya vyuma chakavu,Mpango wa kuunda bodi
mpya ya Tumbaku na Utengaji wa asilimia maalum kwa wanafunzi kutoka
Tanzania Bara na Zanzibar, Ufafanuzi huo umetolewa leo Bungeni mjini
Dodoma.
Kushamiri kwa Biashara ya Vyuma Chakavu
Serikali imesema kuwa,
imekwishaandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu
na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa biashara ya chuma chakavu katika
hatua mbalimbali za uzalishaji,ukusanyaji,usambazaji,uuzaji na
uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa
manufaa ya Taifa.
Hatua hiyo imekuja baada ya
kuongezeka kwa mahitaji ya vyuma chakavu hapa nchini na duniani kwa
ujumla na kubainisha maeneo yaliyoathirika sana kuwa ni mifumo ya
kusafirisha Umeme,Reli na Barabara.
Akifafanua kuhusu hoja hiyo,
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage amesema
Muswada huo umeweka bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika
kuharibu miundombinu.
Aidha Mhe.Mwijage ametoa wito kwa Wananchi wote kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu miundombinu kwa namna yoyote ile.
Mpango wa kuunda Bodi mpya ya Tumbaku.
Serikali imesema kuwa, iko
katika maandalizi ya kuunda Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Tumbaku haraka
iwezekanavyo na Wananchi watajulishwa kupitia tamko la Serikali mara
baada ya taratibu kukamilika.
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo
na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha amesema kuwa, Serukali ilivunja Bodi ya
Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wake.
Ameongeza kuwa, hatua ya
kuvunja Bodi hiyo haihusiani na kusitisha shughuli zinazotekelezwa
katika Kilimo cha Tumbaku kwani wapo wataalamu wanaondeleza utekelezaji
wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la Tumbaku nchini.
Aidha kwa kuzingatia kuwa
wakulima wanahitaji huduma muda wote hasa kipindi hiki cha kuelekea
masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18,Serikali kupitia mrajis wa vyama
vya Ushirika nchini imeshateua timu nyingine ambayo ipo Mkoani Tabora
ikiendelea kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ya wakulima ikiwa ni
pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao.
Serikali kuendelea kutenga fedha kwa wahitaji wa Mikopo ya Elimu ya juu.
Serikali imesema kuwa
itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya
juu kwa kuzingatia Sheria,kanuni na taratibu na miongozo itolewayo mara
kwa mara na serikali kupitia bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya
juu.
Naibu Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Stella Manyanya amesema kuwa
utoaji wa Mikopo unazingatia muombaji awe raia wa
Tanzania,muhitaji,mlemavu au yatima na mabaye amedahiliwa katika elimu
ya juu na mwenye kuchukua programu za vipaumbele vya Taifa kama Sayansi,
Hisabati,uhandisi wa Gesi na Mafuta, Sayansi za Afya na Sayansi za
Kilimo na Maji.
Aidha Mhe.Manyanya amesema
kuwa katika Mwaka wa 2015/16 Serikali ilitoa kiasi cha Tsh.bilioni 480
kugharamia Mikopo pamoja na ruzuku kwa wanafunzi wapatao 124,358.
Ameongeza kuwa Serikali inalifanyia kazi suala la wanafunzi kutopata Mikopo ili kuongeza idadi ya wanafunzi.
Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.
Tags
Bungeni