Msaidizi
wa Askofu, jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la
maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe
Sokoine wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33
iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya
kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine,
wilayani Monduli.
Mke
wa kwanza wa Sokoine Mama Napono katrika, na wa pili Mama Nekiteto
kulia, wakizungumza na waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe
nyumbani Wilayani Monduli
Msaidizi wa Askofu, Prosper Lyimo
akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha Waziri
Mkuu wa Zamani, Edward Sokoine
Binti wa Sokoine, Namelok na Kaka
yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na wageni wengine walioshiriki ibada
ya kumbukumbu ya baba yao wilayani Monduli.
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
Wake za marehemu wakiwa wanaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
Mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila akiwa anaweka taji katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
Wajukuu wa Hayati Edward Sokoine wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine
Mtoto wa Hayati Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na wageni waalikwa katika misa maalum ya kumuenzi baba yake.
Baadhi ya wageni kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria misa ya kumbukumbuku ya Sokoine.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na mwakilishi wa mkuu wa
Majeshi Tanzania, Brigadia Jenerali, Anderson Ghulila pamoja aliyewahi
kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Balozi Daniel Ole Njoolay
Baadhi ya viongozi walioshiriki
ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa
Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon
Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu, Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa
Njombe, Christopher Ole Sendeka na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne
Maghembe kwenye picha ya pamoja
Wanakwaya wakiandamana kuelekea eneo la ibada tayari kwa Misa Maalum.(PICHA ZOTE NA PAMELA MOLLEL ARUSHA)