SHIKAMOO babu, mimi naitwa Aisha wa Buguruni, natamani sana kuolewa babu
lakini tatizo langu vijana wenzangu hawanitongozi, sanasana natongozwa
na vibabu tu, tena ambavyo vimeshazeeka eti nikawe mke wa pili. Nisaidie
nifanyeje na mimi niolewe na kijana mwenzangu?
JIBU: Matatizo yenu mabinti wa siku hizi hamuamini kama hao vijana
wenzenu siyo waoaji, sisi wazee ndiyo tunaojua kuwalea mabinti wazuri na
wabichi kama wewe.
Mi nakushauri nitafute tuzungumze ana kwa ana huenda nikakupa mbinu
nyingine nzuri tu na pengine utakubali mwenyewe kuwa mke wangu wa pili,
sisi wazee tunajua mambo bwana, hamshangai bibi yenu kaniganda mpaka
leo?
Tags
busara ziro
