LEO kwenye safu hii tutaongelea jinsi ya kupika pilau ya mayai ya
kuchemsha kwa kuyachanganya na viazi. Hapa mayai yanaingia badala ya
viazi.
MAHITAJI
Chukua mchele kilo moja, mayai matano, viungo vya pilau vilivyosagwa,
mafuta ya kupikia, viungo ambavyo havijasagwa vya pilau, pia maji
yaliyochemshwa. Zabibu kavu, vitunguu swaumu na vitunguu maji
vilivyokatwa vipande vikubwavikubwa.
MAANDALIZI
Pilau ya mayai na zabibu kavu mayai yako kisha yakaange mpaka yawe na rangi ya kahawia au ‘braun’.
WAKATI WA KUPIKA
Sasa chukua mafuta, yaweke kwenye jiko, yachemke, baada ya kuchemka weka
vitunguu maji, vikaange mpaka viwe brauni. Baada ya hapo weka kitunguu
swaumu, kikaange mpaka kiishie, ukimaliza weka viungo vilivyosagwa,
kaanga hadi viive vizuri kisha weka mchele, ukaange mpaka uingie viungo
vyote.
Ukimaliza, weka viungo vizima, vikaange kidogo kisha weka maji. Pilau
likishakaukia maji kama limeanza kuiva weka mayai kama unayatumbukiza
ili ukiwa katika hatua ya kupalia mkaa au kuweka kwenye oven, mayai nayo
yachanganyike na pilau lako.
Tags
MAPISHI
