
Vikosi vya Usalama nchini Kenya viko katika hali ya ulinzi mkali na
tahadhari baada ya kupokea taarifa za ujasusi kwamba wanamgambo wamekuwa
wakipanga mashambulizi ya kigaidi wakati au baada ya sikukuu ya Pasaka.
Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, George
Kinoti ambapo ameeleza kuwa wamepokea taarifa za ujasusi zikieleza kuwa
wanamgambo tisa wanapanga mashambulizi, hivyo tayari vikosi vya usalama
vimejiimarisha na kuhakikisha kunakuwa na tahadhari ya juu kudhibiti
mashambulizi yasitokee.
Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi wote kuwa waangalifu kwa hali ya
juu kabla ya sikukuu ya Pasaka na kuripoti shughuli zote
watakazozitiliwa shaka.
Tags
Jeshi la kenya