ya madai ya mumewe ambaye ni staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma
Mkatoliki’ kutekwa na kuteswa kisha kutelekezwa akiwa na wenzake watatu
baada ya siku kadhaa, mke wa jamaa huyo aitwaye Nancy ameacha gumzo
kufuatia ujasiri aliouonesha katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na familia ya Roma, Nancy ambaye ni mama wa
mtoto mmoja aliyezaa na Roma aitwaye Ivan, alionesha ujasiri wa aina
yake kwani alikuwa halali badala yake alizunguka kila kona jijini Dar
akimsaka mumewe, jambo ambalo baadhi ya wanawake wasingeweza kulifanya.
“Nancy siyo wa mchezomchezo, tangu mumewe alipotekwa alikuwa halali.
Alichokifanya aliomba msaada kwa ndugu zake wa kumtafuta mumewe kila
kona hadi alipopatikana.
“Unaambiwa alizunguka kila sehemu bila mafanikio akimtafuta mume wake
tangu aliposikia taarifa za kutekwa usiku wa Jumatano (wiki iliyopita).
“Nancy alianzia Studio za Tongwe Records (Masaki), baada ya hapo
hakulala, alizunguka karibia vituo vyote vya polisi Dar.
Alituma watu hadi mochwari kumuulizia mumewe na wakati huohuo akiviomba
vyombo vya habari kumsaidia hadi mumewe alipopatikana, tofauti na
wanawake wengine ambao wangejifungia tu kusubiri taarifa.
“Unajua watu wengi walikuwa hawamjui Nancy ni mtu wa aina gani lakini
tukio la Roma limemfanya awe gumzo sana kwa ujasiri aliounesha kwenye
kipindi kigumu alichopitia,” alisema mtu huyo wa karibu wa familia ya
Roma. Akizungumza na Amani juu ya ujasiri aliouonesha kwenye tukio hilo,
Nancy alisema kuwa, tukio hilo lilimfanya achanganyikiwe na kujikuta
akihangaika kwenye vituo vingi vya polisi jijini Dar. Alisema kuwa,
kilichokuwa kinamfanya achanganyikiwe na kushindwa kupata usingizi ni
kwamba, kabla, hakuwahi kumpatia taarifa yoyote kama anatafutwa na
polisi achilia mbali kuwa na tatizo na mtu yeyote.
Hata hivyo, Nancy aliwashukuru wadau mbalimbali pamoja na Watanzania kwa
ujumla kumuunga mkono katika jitihada za kumtafuta mume wake hadi
alipopatikana na bado wameendelea kutoa pole hivyo kuonesha upendo
mkubwa walionao kwa baba mtoto wake.
Tags
Roma
