Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak alisema jana kuwa, kampuni hizo
zimekuja kwa majadiliano na sekta za umma kuhusu namna ya kuwekeza.
Alisema wanaosimamia uwapo wa kampuni hizo ni Wizara ya Mambo ya Nje na
Maendeleo ya Kimataifa ya Ufaransa chini ya Wakala wa Biashara wa nchi
hiyo na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Fedha wa Korea Kusini, Song Eon-Seog
amesema wametoa Dola 88 milioni za Marekani kusaidia uboreshaji wa
mazingira kwa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.