Watu waliokuwamo kwenye orodha ya kuhojiwa kuhusu dawa za kulevya na
kutakiwa kufika Kituo Kikuu cha Polisi lakini hawakufika, wametakiwa
kuripoti haraka.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro bila kutaja idadi
alisema jana miongoni mwao wamo walioorodheshwa kwenye orodha
iliyokabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na
Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
“Niwaombe wote waliopokea wito wa polisi waje wahojiwe kwa sababu mtu
akija mwenyewe ni tofauti na akisubiri nguvu ya dola kutumika
kumkamata,” alisema Siro.
Tags
kamanda sirro
