Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama hicho
kitaendelea kufanya mambo kiungwana kwa kuwa Tanzania ni nchi ya amani
na kuwa hakuna CUF ya Maalim Seif wala CUF ya Lipumba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Maalim Seif alisema CUF
inatimiza wajibu wa kutunza amani na iwapo kingetaka kuleta machafuko
basi kingefanya hivyo tangu zamani.
“CUF ni moja. Ni kweli sisi tumekuwa wapole na waungwana, sisi si
tunaambiwa hii nchi ya amani, sisi tunatimiza wajibu wetu wa kutunza
amani. Hakuna chama kinachotunza amani kama CUF” alijibu mara baada ya
kuulizwa na waandishi wa habari.
“The struggle we continue, mtatia ndani Maalim Seif, mtatia ndani
Mtatiro lakini there are so many Maalim Seif’s. Kuna Maalim wengine ni
vichaa,” alisema
Wakati huhuo Maalim Seif aionyooshea kidole Rita
Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad amezungumza na waandishi
wa habari leo na kusema Wakala wa Usajili wa vizazi na vifo, (RITA)
utakuwa umekiuka sheria iwapo utaisajili na kuitambua bodi ya
wadhamini iliyoundwa na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba.
“Sisi tumekuwa wapole sana, tunaona katiba inavunjwa, lakini niseme
kwamba, kama Rita wataisajili bodi ya Lipumba, watakuwa wamekiuka sheria
yao wenyewe. Bodi ipo na imesajiliwa 1993 na tunacho cheti cha
kusajiliwa” alisema
Alisema ni utaratibu kuwa kila kipindi fulani marekebisho hufanywa lakini bodi haifi.
Alisema bodi ya CUF ipo na kama ofisa Mtendaji mkuu wa Rita ataisajili basi ajue anavunja sheria.