MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)
kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora
nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Akizungumza katika hafla ya Tuzo
ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba
serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi
na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa
ufumbuzi.
Alisema mwaka wa kwanza wa
serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta
fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na
matakwa ya sasa ya kukuza uchumi.
Alisema serikali ipo tayari
kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta
binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo
kwenda katika uchumi wa kati.
Makamu wa rais ambaye katika
hotuba yake alikuwa anazungumzia changamoto zinazoikumba sekta binafsi
katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano
inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba
zinamalizwa.
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa
miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia
kero zinazosumgua sekta ili serikali ifanye maamuzi.
Kwa sasa kuna kamati inayoangalia
namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi Wizara ya
Viwanda na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi serikalini.
Akizungumza kumkaribisha Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji ili amkaribishe Makamu wa Rais kuzungumza
na washiriki katika hafla hiyo,Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Shabbir Zavery alitaja changamoto
tisa zinazotia msukosuko ukuaji wa viwanda nchini.
Moja ya changamoto hizo ni
mabadiliko ya mara kwa mara na ya ghafla ya sera au sheria za kibiashara
ambayo huondoa utulivu kwa wazalishaji.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akirejea kwenye meza kuu baada ya kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla
ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Zavery alisema kwamba ufanisi na
utuilivu wa kufanya biashara unategemea sana kutobadilika mara kwa mara
kwa sheria na sera za biashara na mwaka uliopita serikali ilichukua
maamuzi kadhaa bila kuhusisha sekta binafsi na hivyo kudhoofisha
ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara.
Pia alisema kwamba utitiri wa
mamlaka za udhibiti na tozo zao mbalimbali pia kufanyakazi zinazofanana
na kutembelea viwanda kwa kila mamlaka kwa wakati wake kunachangia
gharama za kufanyabiashara.
Akizungumzia tatizo sugu la wenye
viwanda na wafanyabiashara kutorejeshewa malipo stahiki (Vat na
nyinginezo) wanazodai kutoka Mamlaka ya Kodi, na kodi zinazoua
ushindani,Makamu wa Rais Samia amesema kwamba serikali kwa sasa
imeshatulia na kwamba itaendelea kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria
na suala la kodi limeshafanyiwa maelekezo na kwamba wahusika wanatakiwa
kukutana kushughulikia tatizo hilo.
Aidha ameiagiza Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mikakati ya
kupunguza kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara inatekelezwa kwa
vitendo.
“Nafahamu kuwa sekta ya viwanda
imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali. Serikali tunaendelea
kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha viwanda vyetu vinakuwa katika
mazingira rafiki na wezeshi ili kuwaongezea ufanisi na ushindani katika
masoko ya kimataifa” alifafanua Makamu wa Rais.
Makamu
wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery akisoma risala ya
Mwenyekiti wa CTI kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo
ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.Makamu wa Rais alikumbushia maneno aliyotoa katika ziara zake
mikoani kwa taasisi za serikali na sekta binafsi kukaa, kujadili na
kuona namna ya kuondoa adha katika uwekezaji na ufanyaji biashara bila
kuipotezea mapato serikali. Aidha alisema kwamba wakati serikali inaendelea kuchukua
hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zinazoathiri ukuaji wa sekta ya
viwanda, ni muhimi pia kwa wawekezaji na wazalishaji kutambua majukumu
yao katika kuchangia juhudi hizo. Alisema majukumu hayo ni pamoja na kuzalisha bidhaa nyingi, zenye ubora na zenye bei rafiki kwa mlaji. “Tusisahau kuwa sekta ya viwanda ina jumkumu kubwa sio tu la
kuipatia serikali mapato; bali pia kutoa ajira kupunguza umaskini pamoja
na kuijengea nchi heshima kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani
wa kimataifa” alisema Makamu wa Rais. Aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuratibu
na kukutana na wizara au taasisi za serikali na za umma nchini ili
kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kama ilivyoanza
kwa vikosi vya usalama ambapo wanatakiwa kununua bidhaa zao hapa nchini. Pia amewataka wafanyabiashara kuingia ubia na mifuko ya jamii ili kuwa na mitaji itakayowezesha kuanzisha viwanda kwa pamoja. Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga
alipokuwa akiwatambulisha wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kuzungumza katika hafla ya
Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Nalo shirikisho hilo la viwanda limepongeza uongozi wa Serikali ya
awamu ya Tano kwa kufanya uwekezeji mkubwa katika sekta za kiuchumi
zinazotengeneza njia kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Wametaja uwekezaji huo kuwa katika umeme, barabara,reli, maji na bandari.
Katika risala ya CTI kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye
hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016, wamesema
uwekezaji huo utasaidia kushuka kwa gharama za uzalishaji na hivyo
kuongeza ushindani wa wazalishaji wa Tanzania katika soko la ndani na la
nje.
Akisoma risala hiyo kwa Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa Shabbir
Zavery, alisema, pamoja na mafanikio katika miundombinu uwekezaji
uliofanywa katika elimu utasaidia kutoa wataalamu wengi wenye tija
katika sekta ya viwanda ambayo inategemea kukua kwa kasi katika kipindi
kifupi kijacho.
Aidha alisema pamoja na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda,
biashara na uwekezaji taifa katika awamu ya tano imeshuhudia kukua kwa
pato la taifa kwa asilimia 6.75; kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka
asilimia 5.6 mwaka 2015 ukilinganisha na wastani wa asilimia 5.2 mwaka
2016.
Mafanikio mengine aliyoyaeleza Zavery ni kuongezeka kwa mauzo ya nje
ambapo jumla ya dola za Marekani bilioni 9.38 zilipatikana ukilinganisha
na dola za Kimarekani bilioni 8.92 zilizopatikana mwaka 2015.Likiwa ni
ongezeko la asilimia 5.2.
Aidha katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira Bora ya Biashara
ya mwaka 2016 Tanzania ilishika nafasi ya 139 ikilinganishwa na nafasi
ya 140 mwaka 2015.
“Vile vile usimamizi mzuri wa mapato ya serikali umewezesha
kuongezeka mapato ya serikali kila mwezi kufikia zaidi ya shilingi
trilioni moja ikilinganishwa na shilingi bilioni 900 zilizokusanywa
mwaka 2015” alisema.
Alisema hata hivyo pamoja na mafanikio hayo ambayo yamepatikana
katika kipindi kifupi, kuna changamoto ambazo kwa kiasi zinapunguza kasi
ya mafanikio. Mkurugenzi
wa Ishara Consultants Ltd, Isaac Saburi, akitoa maelezo mafupi ya
vigezo vilivyotumika kuwapata washindi wa Tuzo ya Rais ya Mzalishaji
bora kwa mwaka 2016 kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mazingira yasiyo rafiki
kwa kufanyabiashara yanayochangiwa na mabadiliko ya ghafla katika sera
na sheria zinazohusiana na biashara.
Changamoto nyingine ni utitiri wa kodi na tozo , kutorejeshewa malipo
stahiki ya kodi ya ongezeko la thamani,ushindani unaozuiwa na kodi ya
VAT kwa mali ghafi, upungufu wa makaa ya mawe,vibali vya kazi na bomoa
bomoa inayofanywa na kampuni ya reli isiyofuata sheria.
Zavery aliomba serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo ili azma
ya kuwa na Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2020 inafanikiwa.
Katika juhudi za kuhakikisha kwamba kero zinashughulikiwa CTI
imeandika waraka ambao umewasilishwa Wizara ya Viwanda ili kurahisisha
ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Katika hafla hiyo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , Mh.
Charles Mwijage alisema kwamba wataendelea kushirikiana na CTI
kuhakikisha kwamba vikwazo hivyo vinaondoka.
Alisema ipo mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa utitiri wa
mamlaka na kodi ili kuhakikisha kwamba viwanda vipya vinaongezeka na
vile vilivyopo vinashamiri.
Alisema kwa mwaka 2015 hadi 2016 viwanda zaidi ya 2000 vimesajiliwa na mamlaka mbalimbali ikiwamo EPZ, SIDO, NDC na TIC.
Amesema kwamba kwa sasa wizara yake imeweka mkakati mahsusi wa
kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na katika hili wamepanga
kukutana wafanyabiashara mjini Dodoma kutafakari changamoto mbalimbali. Meza
kuu ya kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo mshindi wa kwanza wa jumla alikuwa ni Tanzania
Breweries Limited, akifuatiwa na Mufindi Paper Mills Company Limited na
mshindi wa tatu alikuwa Kioo Limited.
Aidha kulikuwa na washindi katika viwanda vidogo vya kati na vikubwa.
Mshindi katika safu ya viwanda vidogo wa kwanza alikuwa Alliance Life
Assurance Limited kwenye masuala ya fedha na bima na mshindi mwingine
alikuwa ni Prisons Corporation Sole katika biadhaa za ngozi na viatu.
Kwa viwanda vya kati katika hafla hiyo ambayo mdhamini wake mkuu ni
Bank M, mshindi katika ujenzi alikuwa Dharam Singh Hanspaul and Sons
Limited; safu ya kemikali mshindi alikuwa Royal Soap and Detergent
Industiries Limited; katika nishati ,umeme na elektroniks mshindi
alikuwa Tanalec Limited na katika usindikaji wa chakula mshindi alikuwa
Chemi Cotex industries limited.
Washindi wengine viwanda vya kati walikuwa Ital Shoe Limited katika
bidhaa za ngozi na viatu; Chemi Cotex Industries limited katika bidhaa
za metali ;Nyanza Mines (T) Limited katika bidhaa za madini; Hanspaul
Automechs Limited safu ya magari na vifaa vyake; Tanpack Tissues limited
bidhaa za karatasi na makasha na DPI Simba Limited katika safu ya
bidhaa za plastiki.
Kwa viwanda vikubwa washindi katika nafasi mbalimbali ni Tanzania
Breweries limited, Petrolube T limited, Petrofuel T Limited, Alliance
Insurance Corporation Limited, Said Salim Bakhressa, Alaf Limited, Kioo
Limited, Mufindi paper Mills Company Limited, Jambo Plastics na Nida
Textile Mills T Limited.
Washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa kuzingatia ufanisi katika
uzalishaji, mauzo ya nje, uwekezaji katika teknolojia ya kisasa,matumizi
bora ya nishati, utunzaji wa mazingira, afya na usalama wa wafanyakazi,
uwiano wa kijinsia katika uongozi, pamoja na mchango katika jamii. Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye
pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi cheti kwa niaba ya
ITV na RADIO One kwa kutambua mchangao wao wa kurusha LIVE matangazo ya
hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimakbidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso cheti kwa
kutambua mchango wao kwa kuwa mdhamini mkuu wa hafla ya Tuzo ya Rais ya
Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Mama Jacqueline Mengi cheti kwa niaba ya magazeti ya The
Guardian Limited kwa udhamini wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji
Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio
waratibu wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao
ndio waratibu wa tuzo hizo, Teddy Mapunda kwenye hafla ya Tuzo ya Rais
ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (wa tatu kulia)
akiwa amejumuika na marafiki zake, Nancy Sumari Neghesti (kushoto),
Nasreen Kareem (kulia) pamoja na Fausta Kameja (wa pili kushoto) wakati
wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali
nchini waliohudhuria hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka
2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa pili
kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage walipowasili katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji
bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.Kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na
Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Mhe. Charles Mwijage, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini
(TPSF) Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakielekea katika ukumbi wa
Marquee kwenye hoteli ya Serena jana jijini Dar es Salaam ilipofanyika
hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo
kuhusu vifaa mbalimbali vya umeme kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa
AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi alipotembelea banda la maonesho la Kilimanjaro
Cables linalomilikiwa na kampuni hiyo wakati wa kwa hafla ya Tuzo ya
Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo
kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly ndani
ya banda la kampuni hiyo maarufu kwa utengenezaji wa samani za ndani
kwenye kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi
akimsikiliza Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na
Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (aliyeketi) wakati akitoa maoni juu ya
ubora wa samani hizo za ndani zinazotengenezwa na Kampuni ya Amorette
Ltd inayomilikiwa na Bi. Jacqueline Mengi (hayupo pichani) katika hafla
ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katibu
Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt.
Adelhelm Meru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda
Tanzania (CTI), Leodegar Tenga wakitia baraka kwenye banda la maonesho
la Kampuni ya Amorette Ltd katika kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya
Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.Afisa
Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (kulia) akiwa na
wafanyakazi wenzake kwenye banda la maonesho wakati hafla ya Tuzo ya
Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti
mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa
kampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh Hanspaul (kushoto) kabla ya kuanza
rasmi kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhelm Meru.Mkurugenzi
Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (kulia)
akifurahi jambo na rafiki yake Fausta Kameja katika hafla ya Tuzo ya
Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo za CTI,
Teddy Mapunda (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kushoto
aliyesimama) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa
mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti
mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kulia)
wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016
iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Mshehereshaji
wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Bw.
Innocent Mungy (wa pili kulia aliyesimama) akifafanua jambo kwa wageni
waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika
Hoteli ya Serena.Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (wa pili
kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline
Woiso (kulia) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya
Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk.
Reginald Mengi mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena
kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd,
Jacqueline Mengi alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya Tuzo
ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta
Kelly (wa pili kushoto) alipotembelea banda ya kampuni hiyo
inayojishughulisha na utengeneza wa samani za ndani (Furniture). Wa pili
kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline
Mengi pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles
Mwijage (aliyepo pembeni ya Makamu wa Rais).Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi (wa pili
kushoto) alipotembelea banda Kilimanjaro Cables wauzaji wa vifaa vya
umeme ambao walieleza wako mbioni kufungua kiwanda cha kutengeneza
Transfoma za umeme nchini na kuongeza ajira. Kushoto ni Meneja Utawala
wa kampuni ya AFRiCAB Group, Kunajal Gina na Katikati ni Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji
Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya CTI.Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake walioshiriki kwenye hafla ya
Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.