Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni
ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu
mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia
kuokoa uharibifu wa Mazingira.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es salaam,
amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya
Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.
Amesema kuwa uharibifu unafanywa
kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo
unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za
kiuchumi.
Aidha, Makamba amewataja Mawaziri
watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji,
Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.
Vile vile, ameongeza kuwa hali ya
mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati
wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa
zamani.
“Hali hii inasababisha kupungua
kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao
unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu
wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,”amesema Makamba.
Hata hivyo ametoa wito kwa
wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea
manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.
Tags
MAZINGIRA