Mwakilishi wa benki ya CRDB
akimpongeza muogeleaji nyota wa Tanzania anayesoma Uingereza kwenye
shule ya St Felix baada ya kushinda medali ya dhahabu.

Muogeleaji wa Tanzania anayesoma shule ya St Felix,Collins Saliboko ‘ akipambana’ katika mashindano ya Taifa.
Waogeleaji wakionyesha staili ya kuchupa ‘diving’.

Hilal Hilal akichapa maji kwenye mashindano hayo

Peter Itatiro akionyesha staili ya backstroke katika mashindano hayo

Kocha wa Dar Swim Club, Michael Livingstone akisimamia mazoezi ya kupasha viungo moto kwa Waogeleaji wake.

Adil Bharmal wa Taliss akipambana katka staili ya Breastsroke

Reuben Monyo wa Dar Swim Club akionyesha uwezo wake katika mashindano hayo

Romeo mihaly wa Champion Rise akipozi na Tan Liu wa Taliss na Saffiro Kweka wa DSC baada ya kushinda medali.

Collins Saliboko akipozi na wenzake baada ya kushinda medali.
Na Mwanishi wetu
Klabu kongwe ya mchezo wa kuogelea
Tanzania, Taliss imeshinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya
kuogelea ya klabu bingwa yaliyofanyika kwa siku mbili kwenye bwawa la
kuogelea la Hopac, Kunduchi jijini.
Klabu hiyo imejikusanyia pointi
3,587 katika mashindano magumu na ya kusisimua yaliyoandliwa na Chama
Cha Kuogelea nchini (TSA) na kudhaminiwa na Davis & Shirtliff, CRDB
Bank, Mediterraneo Hotel & Restaurant, Coca Cola, Aggrey &
Clifford na The Terrace.
Katibu Mkuu wa TSA, Ramadhan
Namkoveka amesema kuwa Taliss iliweza kujikusanyia pointi 1,681 kwa
upande wa waogeleaji wa kike wakati kwa upande wa waogeleaji wa kiume,
klabu hiyo ilipata pointi 1,886.
Namkoveka alisema kuwa nafasi ya
pili ilichukuliwa na klabu nyota ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC)
kwa kupata pointi 2,587 . klabu hiyo ilipata pointi 1,564 kwa upande
wa wanawake na pointi 663 kwa upande wa wanaume.
Nyota kadhaa wa mchezo huo nchini
chini ya muogeleaji namba moja nchini kwa upande wa wanawake, Sonia
Tumiotto na wenzake, Smriti Gorkarn, Celina Itatiro, Anjan Taylor na
Maia Tumiotto waliweza ‘kufunika’ katika mashindano hayo kwa kuwa na
‘kasi ya ajabu.
Klabu ya Morogoro maarufu kwa
jina la Mis Piranha ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupata pointi
1,434. MIS ilipata pointi 606 kwa upande wa wanawake na jumla ya pointi
828 kwa upande wa wanaume.
Waogeaji wa klabu ya Mwanza (MSC)
walishika nafasi ya nne kwa kupata pointi 1,122 huku klabu ya Zanzibar,
Wahoo ikimaliza katika nafasi ya nne kwa kupata pointi 497. Nafasi ya
tano ilichukuliwa na klabu ya Bluefins kwa kupata pointi 442 wakati
Champion Rise ikiibuka ya sita kwa kupata pointi 221.
Klabu za Moshi iliopata pointi,
KMKM, Kennedy House School, Zanzibar Dolphins, , Heaven of Peace academy
na JKT zilimaliza katika nfasi ya saba mpaka ya 13.
Namkoveka alisema kuwa mashindano
hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na maandalizi mazuri na
sapoti kutoka kwa wadhamini.
“Tunashukuru kumaliza salama
mashindano haya, kwa kweli yalikuwa magumu na kwa mara ya kwanza, jumla
ya waogeleaji 172 walishiriki, hii ni ishara kuwa mchezo wetu unakuwa na
tunatarajia kupata mafanikio zaidi katika timu zetu za taifa,” alisema
Namkoveka.
Tags
KUOGELEA