Timu ya Taifa ya Vijana U17
Serengeti Boys imefanikiwa kuifunga timu ya Taifa ya Vijana U17 ya
Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mjini Yaunde Cameroon
usiku huu ambapo mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Ally King’azi
ameifungia timu hiyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Akizungumza kwa njia ya Simu
Mtangazaji wa Kituo cha Redia cha EFM Bw. Maulid Kitenge ambaye alikuwa
shuhuda wa mchezo huo amesema vijana wa serengeti Boys wamecheza vizuri
kama walivyoonyesha mchezo mzuri katika michezo ya awali na leo pia
walionyesha kiwango kizuri cha mchezo na ndiyo maana wenyeji Cameroon
pamoja na kwamba walikuwa nyumbani lakini wamelala goli 1-0 jambo ambalo
linastahili kupongezwa na kila mtanzani kutokana na kujituma kwa vijana
wetu Serengeti Boys.
Timu ya Serengeti Boys imeonyesha
uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali iliyocheza iwe ya mashindano au
ya kirafiki ambapo hivi karibuni imeweza kufanya vizuri katika michezo
yake kwa kutoka sare ya magoli 2-2 kwenye uwanja wa Taifa na timu ya
taifa ya Vijana ya Ghana, ikaifunga timu ya taifa ya vijana ya Gabon
2-0 mara mbili na leo imeweza kuifunga timu ya taifa ya vijana ya
Cameroon 1-0 nyumbani kwao hili ni jambo la kuwapongeza vijana wa
Serengeti Boys kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mchezo.
Baada ya Mchezo wa leo Serengeti
Boys itaelekea nchini Gabon kwa ajili ya kambi tayari kwa kushiriki
michuano ya AFCON U17 inayotarajiwa kuanza mwezi Mei tarehe 14 na kama
timu hiyo itafanikiwa kushinda michezo miwili tu basi itakuwa imekata
tiketi ya kushiriki michuano ya Kumbe la Dunia kwa vijana (World Cup
U17) itakayofanyika nchini India kuanzia tarehe 6–28 mwezi wa 10/ 2017 ikishirikisha timu 24.
Tags
SERENGETI BOYS