Na.Alex Mathias
Timu ya Simba imepunguzwa kasi
kwenye mbio za ubingwa baada ya kutandikwa mabao 2-1 toka kwa Kagera
Sugar mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini
Bukoba.
Alikuwa kinda wa Taifa Stars
ambaye Simba walimlea Mbaraka Yusuph aliifungia Kagera Bao la uongozi
dakika ya 27 kwa shuti kali lililomshinda Mlinda mlango wa Simba Daniel
Agyei kwa makosa ya mabeki ambao walishindwa kujipanga vizuri.
Licha ya kufungwa Simba
waliendelea kulishambulia lango la Kagera uzoefu wa Mlinda mlango Juma
Kaseja umewafanya Simba kukosa ushindi kutokana na kuwa man of the Match
kwa kuokoa michomo hatari hadi Mapumziko Kagera walikwenda wakiwa mbele
1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu
zote zilifanya mabadiliko na dakika ya 46 kinda wa zamani wa Simba tena
Edward Christopher alipingilia msumali wa pili kwa pasi nzuri ya
Japhet Makalai.
Mzamiru Yassin alifunga bao la
kufutia Machozi kwa Simba dakika ya 61 baada ya kutokea piga ni kupige
kwenye eneo la Kagera Sugar hadi Mwamuzi anamaliza Mpira Kagera
wameibuka na alama tatu muhimu.
Kwa Matokeo hayo Kagera Sugar
wamefikisha pointi 45 na kuwashusha Azam FC kwenye nafasi ya tatu huku
Simba wakibaki kwenye nafasi ya pili kwa alama 55 huku Yanga akishika
usukani kwa alama 56.