Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.
Lilian Matinga (kulia) akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda
alipowasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani
Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2017.
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye
miwani) akiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru
wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo Mkoani
Katavi.
: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na wananchi (hawapo pichani)
waliofika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa
sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani
Katavi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,
Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.
Moudline Castico akitoa salamu toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017
katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
akitoa maelezo ya mwenge wa uhuru 2017 kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe
za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya
Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akitoa
salamu za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati
wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika
viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Wakimbiza Mwenge Kitaifa
wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya
kukabidhiwa mwenge huo kuukimbiza kwa siku 195 katika mikoa 31 ya
Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa
Uhuru leo Mkoani Katavi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akimpa
mkono wa baraka kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw.
Amour Hamad Amour kabla ya kumkabidhi mwenge huo kuukimbiza katika mikoa
31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa
Uhuru leo Mkoani Katavi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi
(wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru
katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe
za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya
Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya
kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge
huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe
za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya
Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Watumbuizaji kutoka Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
…………………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
Wananchi Mkoa wa Katavi wameombwa
kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mheshimiwa
Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa
na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kujenga uchumi wa viwanda
nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo
katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi na kusema
kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni ule utakaolifanya taifa
kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya
kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za viwanda vya mataifa
mengine.
“Tanzania tumeazimia kutoka
katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi wa uchumi wa
viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao utahusisha wadau
mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta binafsi na Mashirika
Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan katika uwekezaji
mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na upatikanaji wa
rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi Iddi.
Aidha Mhe. Balozi Iddi amesema
kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika kujenga na kuendeleza
viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda unaanza kwa jitihada za
wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo
vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa wanazozalisha kila siku
katika maeneo yanayowazunguka.
Akizungumza na wananchi wa Mkoa
wa Katavi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mbio za mwenge wa
uhuru zimekua zikihamasisha amani, mshikamano, kujenga uzalendo na umoja
wa kitaifa kwa kuhamasisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ipo sambamba na malengo ya serikali ya awamu ya
tano ambayo imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda kwa kufufua viwanda
vilivyopo kuanzisha viwanda vidogo vidogo, viwanda vya kati na viwanda
vikubwa.
Mwaka huu, ujumbe mkuu wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru unahusu Mkakati wa kukuza Viwanda nchini, chini ya
Kauli Mbiu isemayo:- “Shiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya
nchi yetu”. Ujumbe huu utaambatana na msisitizo wa Serikali kuhusu
mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa.
Mwenge wa Uhuru uliasisiwa na
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu
na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Hatua hiyo ilikuwa ni
utekelezaji wa ndoto yake iliyotafsiriwa kwa maneno aliyoyatamka mwaka
1958 kwa wajumbe wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria na kuyarudia
tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa
wakati huo akidai Serikali ya madaraka kama Mbunge mwakilishi pekee wa
Tanganyika kwa kusema “Sisi watu wa Tanganyika, tungependa kuwasha
Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya
mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali
palipo na chuki na heshima palipo jaa dharau”.Falsafa hiyo ya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere ujumbe mkubwa kwa Waingereza kwamba, watu wa
Tanganyika wamechoka kutawaliwa.