Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(kushoto) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
(wa pili kulia) wakati akikagua kikosi cha timu ya netball ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya timu ya netball ya Bunge la
Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa
Jamhuri Mjini Dodoma.
Mchezaji wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwenye jezi ya rangi ya bluu bahari, akifunga goli
dhidi ya timu ya Bunge la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo wa netball
uliochezwa leo katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu ya netball ya
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jezi ya rangi ya bluu bahari),
wakipambana na wachezaji wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar (jezi
orange), katika mchezo wa netball uliochezwa leo katika uwanja wa
Jamhuri Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Tags
MICHEZO