Kikao cha kamati ya masaa 72
kilichokaa Ijumaa April 7, 2017 kwenye ukumbi wa ofisi za shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kujadili rufaa mbalimbali ambazo zilitokea kwenye
ligi kuu na michezo ya Play off ya SDL kimemalizika Salama.
Kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu
ni rufaa ya Simba Kwa Bodi ya ligi wakidai wapewe pointi za mchezo dhidi
ya Kagera sugar uliochezwa Jumapili iliyopita na Simba kufungwa Kwa
magoli 2-1. Simba walimkatia rufaa mchezaji Mohamed Fakhi wa kagera
Sugar wakidai alicheza akiwa na kadi tatu za njano na hivyo Kagera
kukiuka taratibu na kanuni za ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
Kamati ya Masaa 72 imetoa ufafanuzi kuwa Maamuzi ya rufaa ya Simba dhidi ya Mohamed Fakhi yatatolewa Alhamisi ya wiki Ijayo.
Tags
SIMBA SC