Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi
hiyo, Jumamosi Aprili 8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda ya
Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Majimaji ya Songea
itaialika African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini
Songea mkoani Ruvuma.
Mechi nyingine kwa siku ya
Jumamosi Aprili 8, mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na JKT Ruvu
kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera wakati wakati siku ya Jumapili
Aprili 09, mwaka huu Stand United itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Ligi inatarajiwa kuendelea
Jumatatu Aprili 10, mwaka huu kwa michezo miwili ambako Simba itakuwa
mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa
Sugar itaialika Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA