Vipo vifungo vingi ambavyo vinaweza kukufunga na kukupotezea mafanikio
yako. Vifungo vingine unavijua na vingine unaweza ukawa huvijui. Kwa
mfano;-
Acha kujiweka kwenye vifungo vya kidini na kuamini utajiri mkubwa ni
dhambi. Kumbuka, mafanikio hayana uhusiano moja kwa moja na kutenda
mabaya.
Acha kuamini umaskini ndio ni kitu kizuri kwako. Hivyo ukashindwa kuweka
juhudi zako zote kwa kisingizio cha kwamba ukiwa maskini ni sawa kwako.
Acha kuamini ukiwa na pesa nyingi ndio ushetani. Utajikwamisha sana wewe
mwenyewe kufikia mafanikio yako bila kujijua ukiwa upo kwenye kifungo
cha dini.
Acha kuamini kwamba Mungu atakusaidia kila kitu, hata kama umebweteka na
wala hujitumi sana yaani huweki juhudi sana, ndio maana amekupa akili
ufikirie na vingine.
Acha kutumia uvivu wako kutumia kama kisingizo ukiamini hio ndiyo imani
sahihi.. Kama kuna kazi unayotakiwa kufanya, fanya kweli. acha
kuendekeza uvivu unaomba kazi kwenye kampuni moja halafu unamlaumu
Mungu. Ukiona uko hivyo ujue kabisa upo kwenye kifungo..
Toka kwenye kila aina ya vifungo ambavyo unaona vinakukwamisha
kufanikiwa sana kwenye maisha yako, kuwa huru ili utengeneze mafanikio
yako.
