
Nimekuwa nikisoma "comments" nyingi sana zinazohusu kutekwa kwa Roma
Mkatoliki na nyingi kati ya hizo comments zinamlaumu Rais Magufuli na
Serikali yake. Hata alipopotea Ben Saanane, watu walikuwa wanaishutumu
Serikali ya Rais Magufuli.
Mimi ningependa kuhoji; hivi ninyi mnaoishutumu Serikali mna uhakika gani kuwa Serikali ndiyo inahusika na mambo haya?
Binafsi naamini na ninatambua wazi kuwa hakuna uthibitisho wowote ule unaoonyesha kuwa Serikali ndiyo inahusika.
Serikali yoyote ile duniani huwa na maadui. Hakuna Serikali isiyokuwa na
maadui hapa duniani. Hata Serikali yetu inayoongozwa na Rais Magufuli
pia ina maadui. Maadui hawa hawapendi kuona Rais wetu Magufuli
anaendesha nchi hii kwa amani na mafanikio. Maadui hawa watafanya kila
wawezalo ili kumchafua Rais na Serikali yake mbele ya macho ya
Watanzania na mbele ya jamii ya kimataifa pia.
Inavyoonekana sasa hivi, maadui hawa wanatumia nafasi iliyojitokeza sasa
hivi hapa nchini au mwanya uliojitokeza kufanya uhalifu kwa kisingizio
kuwa Serikali ndiyo inahusika. Kuna watu wako tayari hata kutoa roho za
wenzao ili mradi tu malengo yao yafanikiwe.
Mimi nina mashaka sana tena sana na baadhi ya vyama vya upinzani hapa
Tanzania. Vyama hivi vikiongozwa na chama fulani hivi, vinaendesha siasa
chafu sana hapa nchini ili tu kuhakikisha taswira safi ya Serikali ya
Rais Magufuli inachafuliwa kwa gharama yoyote ile.
Kuna baadhi ya waliokuwa viongozi wakubwa tu hapa nchini waliokuwa
kwenye madaraka nyeti, sasa hivi wako kwenye upande wa upinzani na
viongozi hawa siyo "MALAIKA". Ni watu wenye uchu wa madaraka, ni watu
wenye mbinu chafu sana za kutafuta madaraka, ni watu wa kufanya siasa za
"matukio" na "maigizo". Watu hawa ni hatari sana kuliko tunavyofikiria,
ni hatari sana tena sana.
Nafahamu kuna baadhi yenu mtatukana sana hapa, lakini amini nawaambieni, ukweli utafahamika na mtabaki midomo wazi.
Kila serikali hapa duniani ina namna ya kuwashughulikia watu wenye
kuhatarisha uwepo wa serikali husika. Hata Serikali yetu pia ina namna
ya kuwashughulikia watu wenye kuhatarisha usalama wa nchi hii, lakini
siyo Roma wala siyo Ben saanane. By the way who is Roma Mkatoliki to the
government? Roma is no body.
Kama ni kuwashughulikia watu, basi mimi nafikiri Lissu angekuwa wa
kwanza, tena siku nyingi sana na siyo Ben Saanane au Roma. Kama ni
kuwafunga midomo watu, basi Lema angeshapotezwa siku nyingi sana na siyo
Roma. Msijidanganye, kati ya hao niliowataja hakuna mwenye uwezo wa
kujificha ama kujilinda iwapo Serikali itaamua kwa dhati kumshughulikia
na kumpoteza mazima! Hakuna mwenye uwezo wa kujilinda hata awe nani.
Watanzania kuweni makini sana na mambo yanayofanyika sasa hivi hapa
nchini. Msikimbilie kumtukana na kumlaumu Rais Magufuli kumbe chawa
anayewatafuna mmembeba wenyewe kwenye nguo zenu.
Serikali inalitambua hili na inajua ni nani anayehusika na mchezo huu
mchafu na It's just a matter of time, kila kitu kitajulikana. Serikali
ina mkono mrefu sana na mbinu hii inayotumiwa na "MAADUI" imeshajulikana
na sasa hivi kuna kazi maalumu "inaendelea". Kazi maalumu ambayo wewe
au mimi hatutatangaziwa au kujulishwa ni namna gani inafanyika.
Rais Magufuli, wewe piga kazi na wala usiyumbishwe na mbinu chafu za
hawa wahuni wachache wanaotaka kukumaliza. Tuko pamoja na wewe Rais wetu
mpendwa.
Tags
RAIS MAGUFULI