Nidhamu ikizidi inakuwa Uoga. Na uoga ni sumu katika maisha ya binadamu yeyote.
Kuna kitu katika sakata hili la North Korea na America, linapaswa kuwa funzo katika dunia hii ya leo.... :
1.Nidhamu ya uoga ni adui namba moja katika maisha yako.
2.Ukitaka kupigana na adui usiangalie nyuma bali mtazame usoni.
3.Njama ikizidi Vita itakuwepo, haiepukiki.
4.Adui akizidisha mashambulizi tafuta njia ya kujihami.
Huyu ndie Rais wa Korea Kaskazini mwenye umri mdogo lakini ana jeuri
kuliko kiongozi yeyote duniani.Msimamo wake usiotetereka umemfanya Trump
aombe suluhu, mimi binafsi vita siipendi ila mpaka hapa katoa somo.
Trump kumbe alitaka ku attack psychologically akiamini dogo ataweka
silaha chini kinyume chake mambo yamekuwa mambo ameambiwa ajaribu aone
mziki wake. Trump kaufyata mkia wa mbele.
