Siku chache zilizopita mwanamuziki maarufu wa miondoko yakufokafoka
almaarufu Roma mkatoliki aliripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana
katika studio za Tongwe record zinazomilikiwa na kijana jina maarufu (J
mada),inasemekana ilikuwa ni majira ya usiku wavamisi walipowasili
katika viunga vya ilipo studio hizo.
Kulingana na maelezo yaushaidi uliotolewa na shuhuda (the city)
mwanadada aliyefika muda mchache kabla gari lawatekaji kuondoka alisema
"ilikuja Noah nyeupe na wakashuka watu watatu,baada ya hapo
wakatuamrisha mimi,bin Laden na wageni kutoka morogoro tuingie ndani ya
geti,tulipoingia ndani ya geti walituuliza kwamba tumemkuta junior au
tumemkuta Roma,tukasema junior hayupo ila Roma yupo ndani,wakatuamrisha
Tukamuite Roma,tukamuita Roma,Roma akatoka akaulizwa wewe ndio ROMA na
ilivyoonekana hawakumjua na pia walimuambia simu yake ipo wapi atokenayo
Roma alitokanao sikuweza kujua nini kiliendelea kwa sababu waliongelea
nnje ya gari,walirudi ndani wakamlazimisha binladen aingie studio akiwa
amesindikizwa na mmoja wao na Wakarudi tena wakachukua TV zilizopo
pale,wakatoka na imma walikuwepo wote ndani ya studio,studio ikabaki
tupu,walivyotoka hapo wakaniambia mimi na wageni wengine waliotoka
morogoro tusiende popote na nilichosikia baada ya hapo ni mshindo wa
gari na gari kuondoka "
Fact:katika ushahidi wa shuhuda (the city) umejidadavua watekaji
hawakuwa na haiba yautekaji kwani kiwango Chao cha ustaarabu kilikuwa
juu sana ukilinganisha na watekaji wengine tunaowasikia na hata
kuwashuhudia.
Hoja ya kwanza (1):watekaji waliuliza tumemkuta Roma na wakatuambia
tukamuite?? Niajabu kwa mtekaji kuwa na nidhamu ya namna hii, mara
nyingi hutumia nguvu kuhakikisha wanatimiza lengo Lao,mtekaji gani huyu
anaogopa kuingia ndani anawaambia mashuhuda nendeni mkamuite Roma ??
Hoja ya pili (2):watekaji wakamuuliza Roma,wewe ndio Roma.sikawaida kwa
msanii maarufu kama Roma ashindwe kujulikana tena na hawa watekaji ambao
kwa asilimia kubwa huenda wakawa ni vijana,tena vijana hawa ndio
wapenzi namba moja wa mziki huu wakufokafoka unaoimbwa na Roma ni wazi
na sio rahisi kutokumfahamu Roma.
Hoja ya Tatu (3):watekaji wakaingia ndani na binladen,picha tunayoipata
hapa bado watekaji walikuwa na ustaarabu napo hawakutaka kuingia studio
wenyewe bado waliitaji mtu mwenyeji waingie nae ndani, wavamizi wengi
hutumia nguvu na wakati mwingine huwa hawajali Mali ya waliodhamiria
kumteka hawa waliomteka Roma watofauti sana.viashiria hivi vya ushahidi
wa( the city)unatuonyesha wazi kunamaslahi binafsi yakisanà na wala
siutekaji kama unavyoripotiwa..
Hoja ya 4.watekaji wakatuambia tusiondoke.watekaji baada yakuwachukua
wahusika wakuu waliwaamuru the city na wenzake wasiondoke hii inamaana
bado walitaka kuhakikisha usalama wa studio unakuwa salama hivyo
walionyesha kujali na kudhamini Mali na vifaa vinginee vya studio. hali
isiyo ya kawaida mtekaji kuhakikisha ulizi wa Mali za mtekwaji.
Upande wa mmiliki wa Tongwe record :nae mmiliki wa Tongwe record
aliskika akiongea akisema "usiku wa jana likitokea tukio lakutisha
sana,walikuja watu ambao hawakufaamika wametoka wapi au wametumwa na
nani,bahati nzuri mimi si kuwepo studio,wakamuhoji ROMA baada ya
kumuhoji Roma wakamuhoji na monie ambaye ni msanii wangu pia kutoka
Tongwe record baada yakumaliza mahojiano yao wakaingia ndani studio
wakachukua TV, computer pamoja na kamera"
Maelezo ya mmiliki wa studio na shuhuda namba moja hayatofautiani sana
bado yote yanaukakasi wa kiwango cha ustaarabu wa hawa watekaji.
Hoja watekaji walimuhoji ROMA.ni tanzania pekee watekaji hupata muda
wakuhoji mtekwaji,sidhani kama inaingia akilini kuskia mtekaji anaweza
kufanya interview na mtekwaji,nguvu na ubabe huwa hawana muda wa kuwa
wakarimu na kuchukua maelezo mara zote watekaji hawana huo muda,ili
lililotokea kwa Roma ni maigizo yenye maslahi binafsi.
Kauli ya mkuu wa mkoa mh.Paul makonda.mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa
ulinzi na usalama wa mkoa ni haki na wajibu wake kuhakikisha mkoa
unakuwa salama pamoja na Raia wake,ni haki na sahihi mkuu wa mkoa
kuingilia kati upotevu wa watu wake.
Mh.Makonda aliskika akisema "bado tunayomamlaka yakudhibiti kila aina ya
utekaji na kuhakikisha wanannchi wetu wanaendelea kuwa salama,sambamba
na hilo nawapa imani tu haitafika jumapili tutakuwa tumeshawapata ndugu
zetu wote wanne na mimi naomba kwa dini zetu kwa imani zetu kila mmoja
kokote kule alipo aombe ili tuhakikishe ndugu zetu tunawarejesha wakiwa
salama.
Kutokana na kauli ya mh Paul makonda imepelekea watanzania kijuiliza maswali kadhaa.
Hoja ya kwanza (1).kauli ya haitafika jumapili Roma na wenzake watakuwa
wamepatikana.Niwazi kauli hii ni Tata na ilikuwa na viashiria vya huenda
kuna Jambo muheshimiwa alikuwa analifahamu zaid, tena ukizingatia huwa
anaukaribu na vijana hawa wanaofanya sanaa,nikweli jumapili hajafika na
vijana wamepatikana,mh ni kijana anajua mbinu nyingi za vijana wenzake
wanazotumia kujipatia umaarufu nadhani alishashtukia na akatoa kauli
iliyojipambanua kuna kitu anafahamu.
Hoja ya pili (2).kauli yakuwarejesha Roma na wenzake wakiwa salama nayo
ni moja ya kauli iliyotolewa na mh mkuu wa mkoa tutawarejesha wakiwa
salama kauli hii nayo iliashiria mchezo mzima huenda mkuu wa mkoa
alikuwa anajua mahali alipo mkatoliki.
Uchambuzi wa kauli ya mhusika mkuu (Roma).Roma mara baada yakupatikana
alipelekwa kituo cha Polisi ambapo naamini aliacha maelezo yakutosha.
Roma aliskika akisema " kutokana na mazingira na situation nzima
hatutakuwa na muda mrefu wakuzungumza, kwakifupi tu niwaakikishie mimi
ni mzima mpaka Sa hivi kiafya na kiakili hata monie,bin LadenI wote
tuwazima wa afya,niwaakikishie sisi wote ni wazima tunaendelea vizuri"
Hoja ya kwanza (1).nifuraha kuskia wapo salama ila yapo maswali ya
kujiuliza nini hasa lengo la watekaji je ni kweli watu hawa walitekwa?
ni kweli mtekaji anaweza kuwateka wasipigwe hata vibao kimoja kiasi cha
kuachiwa wakiwa 100% sawa bila jeraha na hata mkwaruzo wowote?
Hoja namba mbili (2).mavazi ya Roma siku anatekwa na siku
anaonekana,siku anatekwa Roma aliripotiwa kuwa alikuwa amevaa t shirt
nyeupe suruali ya blue aina ya Jinsi, ila siku anapatikana alionekana
akiwa na mavazi meusi .Niwazi uko alikokuwepo alipata fursa ya kupata
huduma muhimu kama kuoga na hata kubadilisha nguo bado kuna ulakini wa
aina hii ya utekaji,sio rahisi kwa watekaji kuwa na moyo wa namna hii
vijana wasanaa inaonekana walikuwa bado katika mwendelezo wa sanaa
yao,haingii akilini aina hii yautekwaji kwakweli.
My take.tusishangae na kuskia nyimbo mpya ya Roma katika kipindi cha
mwezi mmoja kutoka sasa,attention aliyokusudia kuipata amefanikiwa kwa
100% otherwise leo atuambie wa Tanzania hoja nzito kutuakikishia ni
kweli alitekwa na sio kutafuta umaarufu kisanaa.
Tags
Roma Mkaotoliki
