
Aliyekuwa muimbaji wa muziki wa taarab nchini na mmiliki wa bendi ya
Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf ambaye aliamua kuachana na masuala ya
muziki na kumrudia Mungu ameibuka sasa kwa kuanza kufanya biashara ya
tofali.
Mzee Yussuf anasema ameamua kufanya biashara hiyo ya tofali za kujengea
nyumba kwa kuwa Mungu ndiye amemtaka afanye biashara hiyo na si kitu
kingine chochote
"Kwa hakika hii ndio biashara 'Allah' ametaka niifanye na mimi nimeanza
kuizowea 'Alhamdulilaah' ukimtegemea 'Allah' hujutii licha ya majaribu
na mitihani. Tupo chanika Taliani weka oda yako popote nakuletea"-
alisema Mzee Yussuf.
Tags
Mzee Yusuph