
Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita
mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10
wamekufa huku nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirwa na
maji.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ametoa taarifa
ya tahmini hiyo jana, Jumanne wakati akizumgumza na waandishi wa habari
jijini hapa.
Wakulyamba amesema katika yaliyotokena na mvua hizo, watu 10
walimepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, kuangukiwa nyumba na
kutumbukia kwenye mashimo ambapo saba kati yao walikuwa wakazi wa
Wilaya ya Korogwe, wawili Muheza na mwingine ni mkazi wa Jiji la Tanga
huku 20 wakijeruhiwa.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, nyumba 44 ziliezuliwa paa, 218 zilizingirwa na maji, 12 zikisombwa na mafuriko.
Amesema wilaya zilizoathirika zaidi ni Korogwe,Tanga na Lushoto huku Pangani,Mkinga na Handeni zikipata athari ndogo.
Kamanda huyo alisema katika mafuriko hayo,barabara zilizopo katika za
Wilaya mbalimbali mkoani Tanga,zimeathirika kwa kubomoka,kuvunjika
makaravati pamaoja na madaraja.
"Kama mnavyoona mvua bado zinaendelea, nawatahadharisha wanaokaa kwenye
nyumba zilizopo mabondeni wasisubiri maji yaingie ili waokolewe, kuna
wakati mwingine uokoaji unaweza kutofanikiwa na kujikuta
mnaangamia,"amesema Wakulyamba.
Tags
mvua kubwa