
TAARIFA KWA UMMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana
Zanzibar katika kikao chake cha siku moja, Mei 2, mwaka huu, imewateua
wafuatao kuwa wawakilishi wa CHADEMA kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA);
1. Profesa Abdalla Safari
2. Salum Mwalim
3. Ezekia Wenje
4. Josephine Lemoyan
5. Lawrence Masha
6. Pamela Massay
Walioteuliwa watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa
taratibu na Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.
Imetolewa leo Jumatano Mei 3, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Tags
CHADEMA