
Diego Costa ameacha mjadala mkubwa kwa mashabiki wake katika Twitter
kutoka na ushangiliaji wake wa kupungia mkono alipofunga bao lake dhidi
ya Middlesbrough ndiyo ishara ya kuaga Stamford Bridge.
Mshambuliaji huyo Mhispania anaonekana kama ataondoka Chelsea mwisho wa msimu huu inavyooneka atatimukia China.
Costa alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Cesc Fabregas
kabla ya kupitisha mpira katikati ya kipa Brad Guzan kufunga bao lake
la 21 msimu huu.
Nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid alishangilia bao hilo kwa
kupungia mkono wa kuaga wakati klabu yake ikiwa katika mazingira mazuri
ya kutwaa taji la tano la Ligi Kuu England.
Marcos Alonso alifunga bao la pili akipokea pasi ya Cesar Azpilicueta na
kupitisha mpira katikati ya miguu ya kipa Guzan kama alivyofanya Costa.
Nemanja Matic alifunga bao la tatu kwa Chelsea na kuielekeza
Middlesbrough katika mlango wa kushuka daraja baada ya kipigo hicho cha
mabao 3-0.
Tags
MICHEZO