
Nahodha msaidizi wa Liverpool James Milner amesema ataugua endapo watakosa nafasi ya kumaliza wane katika Ligi Kuu ya England.
Mliner ameongeza kuwa kuikosa ligi ya mabingwa msimu ujao ni jambo
ambalo hapendi kulisikia masikio mwake. Milner alikosa mkwaju wa penalti
katika mchezo ambao kikosi cha Jurgen Klopp kililazimishwa sare tasa na
Southampton.
Milner ameongeza kusema Liverpool ni timu ambayo inapaswa kucheza ligi
ya mabingwa na sio kwingineko. Hata hivyo amesisitiza kuwa anapaswa
kuwajibika kwa kukosa mkwaju wa penalti kwenye mchezo huo dhidi ya
Southampton.
Tags
MICHEZO