Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa
magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi
zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu
walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.
Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa
asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa
wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa
asali katika tiba mbalimbali.
Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa
madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama
kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya
dini za mashariki za dunia. Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba
asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo
mdalasini.
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali
katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa,
ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja.
Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala kwa mwezi
mmoja.
