BANDA MEDIA BLOG

POLEPOLE ATEMA CHECHE KWA VIONGOZI WABABE NA WASIOJALI WANACHAMA NDANI YA CCM



Katibu wa Itikadi na Uenezi Humfrey Polepole akiimba pamoja na vionzi wa UVCCM kabla ya kuzungumza na wanachama wa jumuia hiyo na kisha kuwapatia vyeti vya kuhitimu Elimu ya Juu  katika vyuo vya mjini Dodoma
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humfrey Polepole akizungumza nao

 
WanaUVCCM waliopo katika shirikisho la vyuo na vyuo vikuu vya mkoani Dodoma wakishangilia jambo kwenye mahafali ya pili ya wahitimu waliyopo katika shirikisho hilo [PICHA NA JOHN BANDA]




Mnec Anthon Mavunde akizungumza katika mahafali hayo

Mwenyekiti mstaafu wa Shirikisho la vyuo vikuu Zainab Abdala akizungumza na wanafunzi hao

Mjumbe Riziwan Kikwete akifurahia jambo wakati akizungumza na wahitimu hao

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Martin Shigela akisisitiza jambo katika hafra hiyo






Na John Banda, Dodoma
 Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi [CCM] Humrey Poleple amesema chama hicho kitawafuta uongozi wenyeviti na makatibu wa mashina na matawi ambao watabainika kupandikiza mabalozi hewa 

Polepole ameitoa  kauli hiyo wakati alipokuwa akiongea kwenye mahafali ya pili ya wanafunzi wa shirikisho la vyuo na vyuo vikuu vya mjini Dodoma ambao ni wanachama wa CCM 

Alisema kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara kwa viongozi wa ngazi za Mwenyekiti, Katibu, Mwenezi na Uchumi na Fedha ngazi za wilaya na mikoa hasa kunapokuwa na vyanzo vya mapato katika maeneo yao hali inayowafanya kutoheshimu wanachama.

"inapofika wakati wa uchaguzi viongozi hao kwa kujua kuwa wanachama wanajua maovu yao basi huomua kutafuta kadi na kukodi watu wa maeneo mengine ili waweze kuwapigia kula wao, ninyi muendao huko baada ya kuhitimu mkipata taarifa tuleteeni na ikithibitika tutawafita kazi wahusika wote", alisema

Aidha Polepole amesema katika mageuzi wanayoyafanya ndani ya CCM mpya ni kuwapandisha mabolozi kuwa na wanachama hai 50 mpaka 150 badala ya nyumba 10 kama ilivyokuwa awali

Awali akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama hicho wa White House Naibu waziri wa Ajira, Vijana na Walemavi Anthon Mavunde amesema Wizara imeanziasha Muongozo wa Uwanajenzi utakaowasaidia wahitimu wa vyuo vikuu kupata mafunzo kwa vitendo bila vikwazo vya waajili

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG